Sunday 27 October 2013

CHAMA CHA WALIMU KANDA YA KUSINI CHA MPONGEZA MKUU WA WILAYA YA TUNDURU.






 


 Na STEVEN AUGUSTINO TUNDURU

UMOJA  wa  Vyama vya walimu Tazania (CWT) kanda ya Kusini
inayoihusisha Mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi
(UWARUMLI)kilichofanyika katika ukumbio wa Klasta ya walimu mlingoti
Wilayani Tundsuru  wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Chande
Nalicho kwa uamuzi wake wa kushika chaki na kufundisha Somo la
Hisabati Katika Shule ya sekondari  ya Mataka.
 

Pongezi hizo zilitolewa na Mwenyekiti wa Mkutano huo, Mwenyekiti wa
(CWT) Mkoa wa Lindi Mwl. Mlami Seba  wakati akifungua Mkutano mkuu wa
Kawada wa wajumbe wa Umoja huo katika  kanda ya Kusini inayoihusisha
Mikoa ya Ruvuma,Mtwara na Lindi  (UWARUMLI)  na kuongeza kuwa Mkuuwa
Wilaya huyo ni Wakutolewa mfano kutokana na kuwa na moyo wa pekee.
 

 Mwl. Seba aliendelea kufafanua kuwa Dc, Nalicho anapaswa kutolewa
mfano kutokana na kuwa na upendo nan i mwana taaluma wa kweli kwa
madai kuwa kwani  wapo Viongozi wengi  ambao baada ya kuchaguliwa ama
kuteuliwa kushika nyadhifa zingine huacha kuzifanyia kazi taaluma
walizozisomea  kwa madai ya kuwa na kazi nyingi za Kitaifa.
 

Mwl.  Seba aliyasena hayo muda mfupi baada ya Kamati ya Walimu
waliokwenda kutembela Shule ya Mataka Sekondari  kwa lengo la
kusikiliza Kero mbali mbali kutoka kwa walimu wa shule hiyo ambao
pamoja na mambo menginen walidai kushtushwa na kitendo cha kumukuta
Mkuu wa Wilaya hiyo akiwafundisha Wanafunzi wa Kidato cha Nne
wanaotarajiwa kufanya Mtihani wa taifa wa kidato mwanzoni mwa mwezi
November mwaka huu.
 

Dc, Chande Nalicho aliahidi kuingia Darasani na kuanza kufundisha Somo
la Hisabati topck ya Acaunts ambayo kila mtihani wa taifa hutoa swali
moja ambalo lina Point 10 kama mchango wake kwa kwa kuanza na
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya kutwa ya Mataka .
 

Dc, Nalicho alisema kuwa ameamua kujitoa kama mwana taaluma ili
kupunguza ikama ya upungufu wa wafanyakazi wa idara ya Elimu ili
kujionea hali hali ya utendaji kazi wa Walimu anaodaiwa kulegalega na
kusababisha Wilaya yake kufanya vibaya katika matokeo ya wanafuzi
waliofanya mtihani wa kumaliza daraza la saba mwaka 2012.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO