Thursday 6 August 2015

HABARI ZA AFRIKA NA ZA KIMATAIFA ZILIZOTIKISA LEO





Serikali ya CAMEROON imesema wapiganaji wa kikundi cha BOKO HARAM cha nchini NIGERIA wamewateka nyara watu 135, kaskazini mwa CAMEROON. Wapiganaji hao pia wamewaua watu wengine wanane katika eneo hilo.

Wapiganaji wa kikundi cha BOKO HARAM mara kadhaa wamekuwa wakifanya mashambulio ya kigaidi nchini NIGERIA, na katika nchi jirani na hivyo kuhatarisha usalama katika nchi hizo. Viongozi wan chi za AFRIKA Magharibi, walikubaliana kuunganisha majeshi yao ili kupambana na wapiganaji hao wa kikundi cha BOKO HARAM.

 Hata hivyo wapiganaji hao wamekuwa wakiendelea na mashambulio dhidi ya raia katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Wiki iliyopita rais MUHAMADU BUHARI, wa NIGIERIA, alikwenda nchini CAMEROON, kuomba msaada zaidi ya kijeshi ili kuwadhibiti wapiganaji hao wa kikundi cha BOKO HARAM.

Serikali ya MISRI inatarajia kupanua mfereji ya SUEZ, unaotumika kupitishia meli kubwa za kibiashara kutoka barani ULAYA kwenda katika maeneo mengine ya dunia.

MISRI imedhamiria kupanua mfereji huo, ili kuongeza idadi ya meli zinazosafiri kupitia mfereji huo na kuliongezea taifa hilo pato. Kupanuliwa kwa mfereji huo pia kutasaidia kupunguza misululu ya meli zinayosubiri kupita katika mfereji wa SUEZ.

Ujenzi wa mfereji huo unaotarajiwa kuanza leo ALHAMIS utagharimu YURO Bilioni SABA. Mfereji wa SUEZ unaoziunganisha bahari za MEDITERANIAN, mto NILE na hatimaye kuelekea kwenye yaSHAM ni kiungo kikubwa kati ya nchi za ULAYA na ASIA.

Vikosi vya ukoaji vya nchini ITALIA, vikiongozwa na jeshi la majini la IRELAND vinaendelea na zoezi la uokoaji katika bahari ya MEDITERANIAN baada ya boti iliyokuwa imebeba abiria zaidi ya 600 kuzama baharini.

Hadi sasa waokoaji wamefanikiwa kuwaokoa watu 400 wengi wao wakiwa wanawake na watoto.  Watu 25 wamethibitika kufa katika ajali hiyo iliyotokea karibu na pwani ya LIBYA na watu hao walikuwa ni wahamiaji waliokuwa wakielekea barani ULAYA.

Wokoaji wanasema, zoezi hilo linakabiliwa na changamoto kwa waokoaji kutojua idadi kamili ya watu waliokuwa wakisafiri ndani ya boti hiyo.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani-  UNHCR ,MELISSA FLEMING amesema idadi kubwa ya wahamiaji wamekuwa wakikimbia vita na machafuko katika nchi zao

Polisi nchini KENYA wamewaachia huru wanafunzi TISA, kati ya wanafunzi KUMI NAMMOJA waliotiwa nguvuni kwa tuhuma za kuchoma bweni katika shule ya sekondari ya wavulana, wanayosoma ya STEPH JOY.

Polisi pia wamewafungulia mashtaka ya kuhusika na vifo, wanafunzi watatu wa shule hiyo waliokamatwa mapema wiki hii. Wanafunzi watatu wa shule hiyo ya sekondrii ya STEPH JOY, walikufa baada ya bweni lao kuchomwa moto.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo alilazimika kukimbizwa hospitalini baada ya kupoteza fahamu, kutokana na mshituko wa tukio hilo. Polisi wanasema moto huo haukutokana na hitilafu ya umeme, bali uliwashwa kwa makusudi na watu.




Baadhi ya ndugu na jamaa za watu waliokufa baada ya ndege ya MALAYSIA, MH 370 kupotea katika mazingira ya kutatanisha mwaka jana, wanasema hawaamini kwamba mabaki, ya ndege hiyo yamepatikana katika bahari ya HINDI.
Watu hao, kutoka CHINA wanataka serikali ya MALAYSIA kuwapatia maelezo ya kutosha kuhusiana na ndugu zao. 

Idadi kubwa ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni raia wa CHINA na wanasema hawaamini kama bawa na ndege lililookotwa katika visiwa vya RE-UNION ni la ndege hiyo.

Waziri mkuu wa MALAYSIA, anadai kuwa mabaki kipande cha bawa hilo lililookotwa ni sehemu ya ndege hiyo iliyopotea mwaka jana, na hakupatikana hadi leo. Amesema kupatikana kwa ndege hiyo kutasaidia kubainisha kile kilichotokea kabla ya ndege hiyo kuanguka.

Zaidi ya watu 15 wamekufa na wengine 20 kujeruhiwa nchini SAUD ARABIA, baada ya mtu mmoja kujitoa mhanga ndani ya msikiti mmoja. Habari zinasema idadi kubwa ya watu wanaopendelea kuswali katika msikiti huo ni askari wa kikosi maalum cha jeshi la SAUDI ARABIA.

Tukio hilo limetoka katika jimbo la ASIR, linalopakana na nchi jirani ya YEMEN. Habari zinasema milipuko mingine miwili ilitokea ikiambatana na mlipuko huo wa mskitini.

Ingawa hadi sasa hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika na tukio hilo, lakini wapiganaji wa kikundi cha IS na wale wa kikundi cha HOUTHI cha nchini YEMEN wanatuhumiwa kuhusika.

Mizigo ipatao elfu mbili, iko katika uwanja wa ndege wa BARCELONA nchini HISPANIA, ikisubiri kuchukuliwa na abiria, waliyolazimika kuiacha kwenye uwanja huo wa ndege baada ya shirika moja la ndege kufuta safari zake.

Shirika hilo la ndege la HISPANIA linaushutumu uongozi wa uwanja wa ndege wa FUMACHINO, ambao ulilazimika kuufunga uwanja huo ukihofia moto uliotatiza safari za ndege. Moto ulio ulikuwa ukiwaka kwenye msitu, unaopakana na wanja wa ndege wa FUMACHINO, na hivyo kutatiza safari za ndege.

Abiria wanaomiliki mizigo hiyo wametakiwa kwenda kwenye uwanja huo wa ndege kuitambua.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO