Friday 7 August 2015

MAHAKAMA YA MUAGA RAIS JAKAYA KIKWETE





Jaji mkuu OTHMAN CHANDE amempongeza Rais JAKAYA KIKWETE kwa hatua mbalimbali za kuimarisha na kuboresha shughuli za kimahakama na sheria na kuzingatia misingi ya utawala bora.

Akizungumza wakati wa mkutano Rais KIKWETE kuwaaga viongozi na watumishi wa mahakama Jaji CHANDE amesema anamshukuru Rais kwa kufuatilia na kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.

Jaji Mkuu ametaja baadhi ya changamoto zilizopatiwa ufumbuzi kuwa ni pamoja na ujenzi na maboresho ya majengo ya mahakama na ujenzi wa nyumba za mahakimu na kuongeza idadi ya watendaji wa mahakama wakiwemo mahakaimu na majaji.

Aidha pia amempongeza Rais KIKWETE kwa kuweka uwiano mzuri wa uteuzi wa watendaji wa mahakama kwa kuzingatia usawa wa kijinsia ambapo hivi sasa majaji wanawake wamefikia asilimia 41 kati ya majaji wote TANZANIA.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Majaji wa mahakama kuu majaji wafawidhi majaji wastaafu, majaji wakuu wa rufani na majaji viongozi. Waziri wa katiba na sheria, Rais wa chama cha wanasheria Tanzania, wasajili wakurugenzi na watumishi wa mahakama.
@@@@@@@@@



Wadau wa mazingira katika nchi za  Jumuiya  ya AFRIKA Mashariki wametakiwa kushirikiana ili kukabiliana na ongezeko la mmea wa GUGUMAJI ambao unatishia kutoweka kwa viumbe wa majini kwenye ziwa VICTORIA.
 
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Ushirikiamo wa AFRIKA Mashariki Dakta ABDULLA JUMA SAADALA   mwishoni mwa ziara yake ya  kutembelea kituo cha kuzalisha wadudu aina ya MBAWAKAVU ambao wanatumika kushambulia mmea wa GUGUMAJI kilichopo katika Chuo Cha Uvuvi  cha NYEGEZI mkoani MWANZA.

Naibu Waziri SAADALA amesema kuwa licha ya wadudu hao kufanikiwa kupunguza mmea wa GUGUMAJI katika ziwa victoria jitihada zaidi bado zinahitajika.



Waziri  wa  Ardhi, Nyumba  na  Maendeleo  ya  Makazi  WILIAM  LUKUVI  ametoa muda wa miezi  Mitatu kwa Halmashauri ya Jiji la MBEYA kuhakikisha  makubaliano  yanafikiwa na wakazi wa  eneo la SISITIRA  kabla ya wakazi hao kutoa maeneo yao ili kupisha  ujenzi  wa  Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia MBEYA – MIST.
 
Waziri LUKUVI  ametoa muda huo mara  baada  ya  kutembelea  eneo  hilo la SISITIRA  ambalo kwa muda mrefu wakazi wake wamekua wakitaka walipwe  fidia  kabla  ya  kupisha  ujenzi wa Chuo Kikuu hicho.

Mara baada ya kuzungumza na wakazi wa eneo hilo,  wa
ziri  LUKUVI pamoja na mambo mengine ametaka kufanyika upya kwa tathmini ya maeneo ya wakazi hao.
@@@@@@@@@@@@@













Zoezi la ukoaji linaendelea katika bahari ya Mediteranian baada ya boti waliokuwa wakisafaria wahamiaji haramu kuzama katika pwani ya LIBYA.

Vikosi vya ukoaji vikiongozwa na jeshi la majini vya IRELAND  pamoja na ITALIA vinaendelea na kazi ya uokoaji ambapo watu 400 wameokolewa wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Katika ajali hiyo watu  25 wamepoteza maisha.

Mmoja ya waokoaji amesema zoezi hilo limekabiliwa na changamoto kutokana kutofahamika idadi kamili ya watu waliokuwa wakisafiri katika boti hiyo.

Wakati huo huo msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani-  UNHCR ,MELISSA FLEMING amesema idadi kubwa ya wahamiaji wamekuwa wakikimbia vita na machafuko katika nchi zao

LEMING amekiri kuwa safari za wahamiaji wanaokimbilia barani ULAYA zimekuwa zikihatarisha maisha yao.
@@@@@@@@@@@










Wataalamu wa ndege kutoka nchi za UFARANSA, MALAYSIA na AUSTRALIA wamegudua kuwa bawa la ndege lililopatikana Magharibi mwa bahari ya HINDI katika visiwa vya REUNION, lilikuwa la shirika la ndege ya MALAYSIA MH 370.

Waziri mkuu wa MALYSIA NAJIB RAZAK amezungumza baada ya matokea hayo na kusema licha ya maumivu watakayopata familia za waathirika uthibitisho huo utatoa uhakika wa kile kilichotokea.

Ndugu wa familia zilizoathirika wamekuwa na mashaka kuhusu uchunguzi huo na   kudai kuwa wanahitaji miili ya wapendwa wao waweze kuwafanyia mazishi ya heshima.

Aidha  serikali ya AUSTRALIA kupitia waziri wake mkuu,TONY ABBOTT imesema ugunduzi huo umetoa mwanga katika kutatua tatizo.

Ndege ya shirika la ndege la MALYSIA MH 370 ilipotea March mwaka jana wakati ikifanya safari zake ikitokea KUALA LUMPAR kuelekea BEIJING na kuuwa  abiria woete  239 kwenye ndege hiyo.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO