Thursday 6 August 2015

RAIS WA ZANZIBAR DKT ALI MOHAMED SHEINAFUNGUA KITUO CHA WANAWAKE CHA UJASIRIAMALI



Rais wa ZANZIBAR Dkt. ALI MOHAMED SHEIN ametoa wito kwa wanawake nchini kuchangamkia fursa za mafunzo yanayotolewa katika kituo cha kufundisha wanawake utengenezaji wa vifaa vya umeme wa jua na ujasiriamali alichokifungua katika kijiji cha KIBOKWA, wilaya ya Kasazini ‘A’, Mkoa wa KASKAZINI UNGUJA.

Akizungumza katika ufunguzi wa kituo hicho, Dkt. SHEIN amesema kituo hicho kinatoa mafunzo kwa wanawake wote hata waliokosa fursa ya kwenda shule ikiwa ni utekelezaji wa mipango ya serikali kuwawezesha wanawake kuimarisha ujasiriamali.

Kwa upande wake, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii,Vijana, Wanawake na Watoto Zanzibar ZAINAB OMAR MOHAMED amesema uzinduzi wa kituo hicho umefungua ukurasa mpya wa harakati za maendeleo ya wanawake.

Kituo hicho kimegharimu shilingi milioni mia moja na ishirini na nne ambapo Serikali ya Mapinduzi ZANZIBAR imetoa shilingi milioni 76 wakati shilingi milioni 48 zimetolewa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wanawake.








No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO