Wednesday 5 August 2015

WATU 30 WAMEKUFA NCHINI INDIA



 Watu 30 wamekufa na wengine 25 kujeruhiwa katika jimbo la MADHYA PRADESH nchini INDIA, baada ya treni mbili za abiria kupinduka. Treni hizo zimepinduka, baada ya mataruma ya reli kusombwa na maji, kutokana na mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo.



Mabehewa yaliyokuwa yakikokotwa na treni hizo mbili yalipinduka, na waokoaji wamekuwa wakiendelea na zoezi la kuwanasua watu walionasa katika mabehewa ya treni hizo, usiku kucha wa kuamkia leo.



Mvua za msimu zilizokuwa zikiendelea kunyesha mfululizo kwa wiki mbili nchini INDIA, zimesababisha maeneo mengi kuwa chepechepe, na hivyo hata mataruma ya reli kushindwa kuhimili uzito wa treni. Shirika la reli la INDIA limesema kuwa, limekuwa likifanya ukaguzi wa mara kwa mara wa reli zake.



Hata hivyo kuna habari kuwa, kingo za bwawa moja kubwa lililoko karibu na njia za reli zilipasuka na kufanya maji yake kusambaa, hivyo na hivyo kutatiza njia za reli. Wakati huohuo




Umoja wa Mataifa umesema, raia wapatao elfu TANO wameuawa nchini AFGHANISTAN katika kipindi cha miezi sita iliyopita. Taarifa iliyotolewa na umoja huo inasema watu waliokufa zaidi nchini humo ni wanawake na watoto.




Mapigano yanayoendelea nchini AFGHANISTAN ni moja kati ya sababu za vifo nchini humo, huku kundi la wapiganaji wa TALEBAN, likishutumiwa. Mtu mmoja aliyehojiwa anasema, mapigano hayo yamesababisha raia kushindwa kupata huduma muhimu za kibinadamu.




No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO