Thursday 6 August 2015

MWENYEKITI WA CHAMA CHA CUF PROFESA IBRAHIM LIPUMBA ATANGAZA KUJIUZULU WADHIFA WAKE.





Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa IBRAHIM LIPUMBA leo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika jijini DSM.




Profesa LIPUMBA amesema amechukua hatua hiyo kutokana na Umoja wa Katiba ya wanananchi UKAWA unaoundwa na vyama vya NCCR MAGEUZI, CHADEMA, CUF na NLD kushindwa kusimamia makubaliano, ambapo amesema atabaki kuwa mwanachama tu katika chama hicho.




Wakati huo huo, Kaimu  Mkurugenzi wa habari uenezi na mawasiliano chama cha wananchi CUF Zanzibar  ISMAIL JUSS LADU  amesema kuwa Chama  cha Wananchi  CUF  hakiwezi kuyumba kwa kuondokewa   na aliyekuwa Mwenyekiti wake Prof. IBRAHIMU  LIPUMBA.




Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Unguja JUSSA amesema maamuzi ya kujiuzulu Prof. IBRAHIMU LIPUMBA ni maamuzi yake binafsi ambayo wanayaheshimu na Chama kitaendelea kusonga mbele. 




Hatahivyo amesema mchango wake  alioweza kuutoa katika kipindi chake cha Uongozi , CUF itaendelea kuuenzi na kuuheshimu licha ya yeye kujiuzulu nafasi hiyo.



Akizungumzia kuhusu suala la umoja wa UKAWA ndio chanzo cha Profesa LIPUMBA  kujiuzulu, JUSSA amesema si kweli kwani maamuzi yote ya Chama yalikuwa yakifanywa chini yake na kushirikishwa vyema .




Hivi sasa Baraza Kuu la CUF limepanga kuanza kufanya vikao vyake ili kuweza kuziba pengo hilo aliloacha Profesa LIPUMBA .
































































No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO