Thursday 14 March 2013

CHINA YAITABIRIA TANZANIA KUPIGA HATUA



1. KINANA NA UJUMBE WAKE KWENYE MNARA WA PILI DUNIANI KWA UREFUaMtumishi katika mnara wa Canton, mrefu kuliko yote nchini China na watatu duniani kwa urefu, Sarah Xie, akimuonyesha mandhari ya jiji la Guangzhou, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, wakati Kinana na ujumbe wake walipopanda hadi mwisho mnara huo wenye urefu wa zaidi ya futi 100, Machi 13, 2013. Wengine Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine shigella. Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). (Picha na Bashir Nkoromo). 3. KINANA NA UJUMBE WAKE NDANI YA MNARAaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakitazama maumbo ya mandhari ya mji wa Guanzhou, China, yaliyopo ndani ya mnara wa Cnton wenye urefu wa zaidi ya mita 100, walipotembelea mnara huo, Machi 13, 2013.  Kinana na ujumbe wake wapo nchini kwa ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). (Picha na Bashir Nkoromo).
10. DK. MIGIRO NA MAOFISA WA IDARA YA MAMBO YA NJE WA DONGGUANSABINA LIU (L) NA SARAH XIEaKatibu wa NEC, Ushirikiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa mjini Magharibi, Yussuf Mohamed Yusuf wakitaza bidhaa zinazouzwa kwenye kilele Mnara wa Canton ambao ni mrefu kuliko yote nchini China ukiwa na urefu wa zaidi ya mita 100, mjini Guangzhou, China. Dk. Asha-Rose Migiro na Yusuf ni miongoni mwa viongozi walioambatana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika ziara ya siku kumi ya kimafunzo kwa mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC). (Picha na Bashir Nkoromo).
13. KINANA NA MIGIRO WAKIWA NA VIONGOZI WA CHAMA CHA WA-TZ WAISHIO CHINA. (L) DAVID CHAMALA (KTB), JOHN LUHEMBA (MKT)-L, ABRAHAM MERISHANI MAKAMU MKT NA ABUBAKAR MWINYI KATB MSAIDIZIaKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wanachama wa Jumuia ya watanzania waishio nchini China

NA BASHIR NKOROMO, DONGGUAN,CHINA

CHAMA Cha Kikomunisti cha China (CPC) kimeeleza matumaini yake kwamba upo uwezekano wa Tanzania kupiga hatua kubwa kichumi kama inajikita kwa dhati katika kuzitumia rasilimali ilizonazo ikiwemo ardhi.
Hayo yalisemwa Machi 13, 2013 na Kamishna wa Maadili na nidhamu wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), jimbo la Donguan, China,  Cuo Jian, wakati akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na ujumbe wake, katika hoteli ya Exhibition Internation mjini hapa.
Jian ambaye pia ni Meya wa jiji la Donguan, alisema, Tanzania kama zilivyo nchi kadhaa za Afrika, inaweza kupiga hatua kiuchumi ikiwekeza juhudi zake katika kuzitumia rasilimali ilizonazo kwa kuwa rasilimali ndiyo msingi wa kwanza katika kuinua uchumi wa nchi yoyote.
Alisema, anatambuwa kwamba Tanzania ni moja ya nchi za Afrika zenye ardhi kubwa, hivyo haina budi juhudi zake za kuinua uchumi kuzielekeza katika rasilimali hiyo ikiitumia kwa kilimo cha kisasa, kujenga viwanda na vitegauchumi mbalimbali ambavyo vitachochea kukua haraka kwa uchumi.
“Hata hivyo nawapongeza Tanzania, kwa hatua mliyofikia sasa katika kukuza uchumi, asilimia sita ya GDP, inaridhisha, la msingi serikali  kuongeza juhudi na kuwahamasisha wananchi kushiriki katika juhudi hizo”, alisema, Jian.
Akijibu swali na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu, ambaye yupo kwenye msafara wa Kinana katika ziara hiyo, Titus Kamani aliyetaka kujua ni nini hasa China ilifanya hadi kuufanya uchumi wake ukue haraka na kuwa nchi ya pili dunia kwa maendeleo, Jian alisema, China imefikia mafanikio hayo kutokana na kuamua kuwekeza kwa nguvu zake zote kwenye rasilimali ya ardhi.
“Zipo njia nyingi za kuweza kuinua uchumi wa  nchi yoyote, juhudi hizo baadhi zinafanana na nyingine ni tofauti kutokana na nchi na nchi, lakini sisi (Wachina) tulifahamu kwamba tuna ardhi kubwa sana, hivyo tukaamua kuimua rasilimali hii kwa kila namna iliyo bora. Licha ya eneo kuwa kubwa lakini tumehakikisha hakuna eneo linaloachwa bila faida”, alisema.
Kwa upande wake Kinana aliupongeza uongozi wa China chini ya chama cha CPC na wananchi wa nchi hiyo kwa kuweza kufanikisha kuinua uchumi wa nchi hiyo kwa kiwango kibwa cha sasa.
“Bila shaka ni uchapakazi usio na kikomo na wakujituma sana kwa pamoja kati ya serikali na wananchi ndiyo maana mmefanikiwa hivi, napenda kuchua fursa hii niwapongeze kwa dhati kwa mafanikio haya, nasi kama nchi rafiki tunapata kiu kubwa kuhakikisha tunafika mlipo au angalau kuwakaribia”, alisema Kinana.
Kinana yupo nchini China akiambatana na ujumbe wa viongozi na maofisa wa Chama kwa ajili ya ziara ya mafunzo, katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kisiasa, na pia kudumisha urafiki wa kindugu wa siku nyingi kati ya Chama Cha Mapinduzi na Chama Cha Kikomunisti cha nchi hiyo.
Katika ziara hiyo Kinana amefuatana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Khadija Aboud, Katibu wa NEC, Siasa na Uhuaisno wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro, Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM, Martine Shigela, Katibu Mkuu wa Jumuia ya Wazazi, Khamis Suleiman Dadi na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Mohammed Yusuf Mohamed.
Wengine ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa,  Jesca Msambatavangu, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu Titus Kamani, Katibu wa CCM mkoa wa Mbeya Maganga Sengelema na maofisa wa Chama. ziara hiyo
Kinana anafanya ziara  hiyo kutokana na mwaliko wa Chama Cha Kikomunisti cha China, na anafanya ziara hiyo ikiwa ni ya kwanza kuifanya nje ya nchi, tangu alipoteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM, Oktoba mwaka jana mjini Dodoma
Chanzo cha habari http://www.fullshangweblog.com

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO