Tuesday 5 March 2013

WAKALA wa Nishati vijijini kupitia wadhamini wa Rural Energy Agency (REA) kukijengea kikosi cha JKT Mlale mtambo wa kuzalisha umeme wa BIYOGESI ambao utakagharimu kiasi cha shilingi milioni 123


Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Joseph Joseph Mkirikiti akisisitiza jambo katika ufunguzi wa mafunzo katika kikosi cha JKT Mlale

Meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew akitoa maelezo mbele ya mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti.
  Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
  Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemoakitoa maelekezo kuhusu mtambo utakao wekwa katika shimo lililochimbwa kwa ajili ya kuweka mtambo.
Shimo hili ni lamtambo utakao wekwa
 ......................................................................................
 WAKALA wa Nishati vijijini kwa kupitia wadhamini wa Rural Energy Agency (REA)wametoa mafunzo ya utengenezaji wa mitambo ya umeme ya Biyogesi kwa kikosi cha JKT MLALE ,842KJ kilichopo wilaya ya Songea mkoani Ruvuma pamoja na kuwajengea mtambo wa umeme huo kikosini hapo  utakao garimu milioni 123 ,ili kufanikisha kukabiliana na tatizo hilo ikiwemo na uharibifu wa mazingira.

  Akiongea jana meneja wa mafunzo na ujengaji uwezo Grace Mathew mbele ya mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia sana katika hali ya kukambiliana na changamoto za ukosefu wa wa Nishati ya umeme pamoja na uharibifu wa mazingira kwa kukata miti kwa ajili ya mkaa na kuni.
 
  Methew alisema kuwa wameamua kutoa mafunzo kikosini hapo kwa kuwa watu wa sekta hizo za JKT ndio wenye uzalendo mkubwa wa kutoa elimu hiyo kwa vijana mbalimbali hasa waliyopo mafunzoni kwenye vikosi hivyo na kuwa vijana hao pia wataenda kutoa elimu hiyo kwa wananchi wengine ikiwemo na kuwatengezea mitambo hiyo ambayo garama yake ni nafuu.

 “Nasema ni garama nafuu kwa kuwa kunamitambo midogo kulingana na uhitaji wa mwanachi mwenyewe anavyohitaji matumizi yake ya umeme huo na kuwa sasa ni zamu ya watu wa vijini kunifaika na hiyo mitambo ya biyogesi na kuachana na tabia ya kuona umeme wanapata watu wa mijini tuu”alisema meneja huyo.
  
  “Vijijini siku zote walikuwa wakitoa michango yao  kwa serikali kupitia  ulipaji  kodi ya vitu mbalimbali ndani mwake kukiwemo na suala la umeme sasa ni wakati wa kuwatambua na wao kuwa wapate umeme ambao hawata kuwa na garama ya kuwajibika TANESCO kama ilivyo kwa umeme unaotumika mijini”alisema.
     
  Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti akisoma hotuba yake wakati akifungua mafunzo hayo alisema kuwa ni vyema sasa suala hilo la umeme wa biyogesi lizingatiwe kwa umakini ili kuondokana na uharibifu unaofanywa katika misitu mbalimbali hapa nchini.
    
   Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa zoezi hilo likifanikiwa litasaidia sana hata kwa vijana ambao kwa sasa wamekosa ajira hivyo kwa kufanya kazi hiyo ya ujenzi wa mitambo hiyo kwao itakuwa ni ajira tosha  na hatimaye watainua uchumi ndani ya Taifa pamoja na uchumi wao .
       
   “Naomba niseme kwa moyo wa dhati umeme wa mtindo huo nimeshauona na nimeona manufaa yake hivyo ningeliomba hata kwa wabunge wetu wawapo mbungeni kuliongelea suala la umeme wa biyogesi kwa wananchi kwa kuwa ni sehemu ya ilani ya utekelezaji wa chama cha Mapinduzi CCM”alisema kuwa kila mwanachi anahaki ya kutumia Nishati hiyo.
          
  “Leo kikosi hiki cha JKT MLALE mnajengewa mtambo wa uzalishaji wa umeme wa biyogesi wenye thamani ya milioni 123 utakao kamilika ndani ya miezi miwili na kupata umeme ambao hauna ugovi na shirika la TANESCO je mngesubiri umeme wa gridi ya Taifa mgepata leo “alisema mkuu huyo wa wilaya.
       
 Alisema kuwa sina maana kuwa umeme wa gridi ya Taifa usifike Songea bali nasema wakati umeme huo unasubiriwa sisi tuwe na umeme mbadala ambao hauna garama ya kutumia na kwamba umeme huo hauna kuweka manguzo bali ni wewe na Nyumba yako.
      
  Naye Meja mkuu wa kikosi hicho Thomas Mpuku alipongeza jidihada zilizofanywa na watu wa Wakala wa Nishati vijijini kwa ubunifu wao mkubwa na kuendesha mafunzo hayo katika kikosi chake na kuwa yeye atahakikisha elimu hiyo inaendelezwa na wengine .

   Aidha Injinia wa Wakala wa Nishati Vijijini Enocent Nyemo ambaye anasimamia ujenzi wa mtambo huo katika kikosi cha JKT MLALE alisema kuwa ukifanikiwa kuwa na mtambo wa biyogesi kazi yako kubwa ni kutumbukiza taka unazo zizalisha kwenye mtambo huo ili kuendelea kupata umeme.

 Hata hivyo alisema kuwa wamesha pita katika maeneo  mbalimbali kutoa elimu hiyo na kujenga mitambo hiyo na sasa tayari wananufaika nayo na pia wataendelea kwenda katika maeneo mengine kutoa elimu hiyo.
    
Picha na habari kwa hisani ya  www.demashonews.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO