Wednesday 6 March 2013

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amepiga marufuku vitendo vya kuchochea vurugu katika mkoa wa Ruvuma katika kikao cha ushauri wa mkoa



 Mbunge wa jimbo la Namtumbo VITA KAWAWA wa kwanza kulia , katikakti ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya namtumbo  bwana kinana
 kulia ni mkurugenzi wa wilaya ya mbinga na mbunge wa jimbo la mbinga mashariki Gaudence Kayombo wakisikiliza jambo katika kikao cha ushauri cha mkoa.




Serikali mkaoni Ruvuma imepiga marufuku kuuza kanda zinazoenezanchuki na kuchochea masuala ya vurugu katika mkoa wa Ruvuma.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amepiga marufuku vitendo hivyo katika kikao cha ushauri cha mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Songea club katika manispaa ya Songea.

Amesema serikali haitamvumilia mtu , kundi au kiongozi yeyote wa dini ama siasa atakayeonekana kuchochea machafuko na chuki miongoni mwa wananchi katika mkoa wa Ruvuma.

Ameongeza kuwa serikali kupitia jeshi la polisi itamkamata mtu yeyote mchochezi na kumfikisha mbele ya sheria bila kujali nafasi yake.

Mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma ametumia nafasi ya kikao hicho kuwaomba wakazi wa mkoa wa Ruvuma kushirikianan na serikali ili kuwafichua na kuwabaini wanaouza kanda za uchochezi za aina yeyote zinazoeneza chuki za kidini.

Aidha amewataka viongozi wa dini ya kiislamu na wakristo kupitia misikiti na makanisa kuhubiri upendo ,amani, na utulivu miongoni mwa wananchi.
Said Mwambungu amewasihi wakazi wa Ruvuma kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano wa kitaifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO