Wednesday 6 March 2013




 Kikao cha kamati cha ushauri cha mkoa wa Ruvuma kimewaagiza viongozi wa kila wilaya kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenda kuripoti shuleni kabla ya mwisho wa mwezi huu.


Agizo hilo limetolewa na wajumbe wa kikao hicho baada ya kupata taarifa kutoka kwa afisa elimu wa mkoa wa Ruvuma Mayasa Hashimu kuwa jumla ya wanafunzi 6300 waliofaulu hawajaripoti shuleni mpaka leo.

Hivyo kikao kikalazika kuwaomba viongozi kila mmoja kutumia nafasi yake kuwabana wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao kuripoti shuleni.

Wajumbe wa kikao hicho wametoa muda kuwa mwisho wa kuripoti wanafunzi wote wasioripoti shule ni tarehe 20.3.2013,
Itakapofika tarehe hiyo kila mkuu wa wilaya anatakiwa kutoa taarifa ya wanafuznzi ambao bado hawajaripoti shuleni na  wazazi wao wamechukuliwa hatua gani za kisheria.

Akizungumzia sakata la wanafuzi wa kidato cha nne kufanya vibaya katika matokeo ya mtihani wao afisa elimu mayasa hashimu amesema baada ya kufanya utafiti amegundua kuna changamoto nyingi sana katika pande zote za wazazi walimu wanafunzi na serikali.

Kwa upande wa wazazi afisa elimu amesema wazazi wengi wanasahau wajibu wa kuona umuhimu wa watoto kwenda shule na kuhakikisha watoto wanhudhuria shule kila siku, kuwaandalia vifaa vya shule kama vitabu na kuhakikisha watoto wao wanapata chakula cha mchana.

Aidha wazazi pia wanatakiwa kutoa michango inayopitishwa na kamati  za shule au bodi ya shule.

Pia wazazi wametakiwa kujenga tabia ya kufuatilia maendeleo ya shule ya watoto wao na kukagua mahitaji yao na kubwa zaidi kuwajenga watoto katika maadili mema kwa kuhakikisha wavaa mavazi mazuri na kuwapatia mahitaji muhimu ya shule.

Afisa elimu huyo aliomba  marufuku  kuwa ngoma ya saka mimba ambayo ipo katika wilaya ya Tunduru ambayo inahamasiha watoto kupata mimba.

Kwa upande wa wanafunzi amewataka wajitambue na wawe na malengo na kujua nafasi yao katika jamii na kujijengea tabia ya kujisomea na kutembelea maktaba.

Akiwageukia walimu amewataka wafanye kazi zao kwa uaminifu, watoe notes zinazoendana na mihutasari,walimu watoro wafikishwe kwenye vyombo vya sheria.

Akizungumzia serikali kuwajibika kwa upande wake kuhusu elimu amesema serikali inapaswa kuwasikiliza walimu matatizo yao na kuwasaidia pale wanapokuwa na shida.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO