Sunday 24 March 2013

TAIFA STARS YAWAZABA LIONS OF THE ATLAS

Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamewainua watanzania kwa kumzaba Morocco mabao 3-1 katika mechi ya kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia.

Mabao ya Taifa Stars yametupiwa na Thomas Ulimwengu katika dakika ya 46 na Mbwana Samatta alizifumania nyavu katika dakika za 67 na 80.

Bao pekee la Lions of The Atlas limefungwa katika dakika ya 90 ya mchezo huo ambao umechezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Pia katika mechi hiyo mchezaji wa Morocco Abderrahim Chakir alionyeshwa kadi nyekundu kufuatia kucheza vibaya.

Kwa matokeo hayo Stars inaendelea kushika nafasi ya pili ikiwa na alama 6 kutokana na Ivory Coast jana kumnyuka Gambia mabao 3-0 na kuwa na pointi 7 ikipisha alama moja tu na tembo hao wa Afrika.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO