Wednesday 24 April 2013

WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA YABAINI VIKWAZO VYA ELIMU






Na Steven Augustino, Tunduru
 

Imebainishwa kuwa Mahusiano mabaya kati ya Walimu na Wanafunzi na
Wanafunzi wadaiwa kukataa kukaa katika mabweni na Hosteli ni miongoni
mwa vikwazo vya maendeleo ya elimu Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma na
kupelekea Wilaya hiyo kupata matokeo mabaya kwa wanafunzi waliofanya
mitihani ya Kidato cha Pili Nne katika kipindi cha mwaka 2011/2012 .
 

Hayo yalibainishwa na afisa elimu Sekondari Mwl. Ally Mtamila wakati
akiwasilisha taarifa ya matokeo ya kidato cha pili na cha Nne
katikakipindi cha mwaka 2011/2012 kuongeza kwa kuwataka wzazi
kushiriki katika usimamiaji wa Watoto wao kuwa nma hamasa ya kupenda
masomo pamoja na kukemea watoto wanaokwepa kuingia darasani ambao
wamekuwa wakiachwa waendelee kucheza wakati wenzao wakiwa darasani
zikiwa ni juhudi za kuinua taaluma kwa watoto wao.
 

Kwa mujibu wa tarifa hiyo mwaka 2011 matokeo ya Kidato cha pili Wilaya
hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 35%, huku takwimu hizo kwa
upande wa matokeo ya Kidato cha Nne katika kipindi cha mwaka 2012
zikionesha kuwa Wilaya hiyo ilifaulisha kwa wastani wa asilimia 59.46%
kiwango kilichodaiwa kuwa ni kidogo na kiliifanya Wilaya yao kushika
nafasi ya mwisho kimkoa.
 

Awali aikifungua Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Tunduru  Chande Nalicho
pamoja na kubainisha kuwa pamoja na serikali kuwa na vipaumbele
vingine vya maendeleo lakini Elimu ni muhimu ilikujiletea mabadiliko
ya kweli.


 Mkuu wa wilaya ya Tunduru Nalicho aliendelea kueleza kuwa Ili kuwaletea maendeleo wananchi wa
Tdr ni lazima wilaya ijikite katika kusimamia elimu na kuhalalisha
uwepo wao na kwamba wasipo wakazania kusomaa shuli maendeleo
yanayopiganiwa na serikali hayatakuwa na maana yoyote kwao.
Katika taarifa hiyo Mkuu Dc. Nalicho akatolea mfano wa Takwimu za
ufaulu wa wanafunzi 2764 waliochaguliwa kujiunga na masomo ya
sekondari  hadi mwishoni mwa mwezi wa tatu ni asilimia 60% ya  watoto
wote waliochaguliwa  kujiunga na masomo ya sekondari.
 

 Akizungumzia upande wa Shule za Msingi  Mwaka 2011Shule ya Msingi
Nakapanya ilifaulisha Watoto 26 lakini takwimu zinaonesha kuwa  watoto
wote hawakwenda shule na kuongeza kuwa hali hiyo inawakatisha tama
hata walimu wa shule za msingi zinazofaulisha watoto hao Serikali
inayo mikakati
 

Wakichangia kwa nyakati tofauti Mwl. Issa Ngajime alisema kuwa chanzo
cha kushamiri kwa utoro,uchangiaji hafifu wa chakula mashuleni na
wanafunzi kukataa kukaa katika hostel zilizojengwa katika shule zao
Viongozi wa serikali za Vijiji wanastahili kubeba lawama huku
wakiwataka viongozi kutochanganya elimu na Siasa kwa kuboresha mbinu
za kufundishia na kuchukua hatua kwa Wanafunzi ambao wamekuwa
wakibainika kuchaguliwa wakiwa hawajui kusoma,kuandika na kuhesabu.
 

 Mkuu wa shule ya Mgomba Mwl. Elis Banda alisema kuwa tatizo wanafunzi
kukataa kukaa katika Hosteli linatokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya
watoto wanaosoma katika shule hizo kuwa ni wakazi wa maeneo husika na
akapendekekeza kuwepo kwa utaratibu wa kutenga Shule za kanda kwa
ajili ya kupeleka wanafunzi kutoka maeeneo tofauti huku akiitaka
serikali kutoa maelekezo ya vitabu vya kununuliwa tofauti na sasa
ambapo kumekuwa na maelekezo ya kuwataka wakuu wa shule kutumia vitabu
kutoka katika kampuni ya EMACK  ambapo alishauri kupunguzwa kwa idadi
ya vitabu vya kufundishia.
 

Wadau hao waliendelea kubainisha vikwazo vingine kuwa ni pamoja na
Muingiliano wa sekula pia ni kikwazo cha Willaya kufanya vizuri kwani
sasa wanalazimishwa kusajiri watoto wote kufanya mitihani bila
kuangalia wakati huo mamlaka zikiwataka walimu kuwafukuza watoto
wasiofika shule katika kipindi cha miezi mitatu  huku serikali wakati
huo ikihamasisha na kuwapeleka shule wanafunzi wa kidato cha kwanza
walichelewa kuripoto Shuleni ni kikwazo kingine ambacho kimekuwa
kikiwafanya walimu kufundisha kwa kulipua na kushindwa kulamiza
silabasi.
 

Ujauzito pia tatizo lakini Bodi za shule zimekuwa zikifanya kazi ya
ziada lakini kila wanapofuatilia matokeo ya kesi Polisi huwa
hawapatiwi majibu ya maendeleo ya kesi husika hali inayo wakosesha
imani.
 

Mkuu wa Shule ya sekondari Lukumbule Mwl. Mathias Katto akabainisha
vikwazo vingine kuwa shule zao kutokuwa na walimu wa masomo ya
Sayansi,Shule kutokuwa na maktaba,Watoto kutoka katika maeneo husika
na miundombinu ya Nyumba wanazoishi n imbovu zinvuja na kwamba siyo
rafiki kwa Walimu.
 

Marafiki hao wa elimu pia wakanyooshea kidole mila na destuli potofu
za kuwafundisha watoto wadogo hasa wa kike mafunzo ya kuishi kiunyumba
ambayo hutolewa kupitia katika jando, Unyago
na Msondo na ngoma ya Sakamimba hali ambayo imekuwa ikipelekea baadhi
ya wanafunzi kuishi kwa wanaume huku wakiwa wanaendelea na masomo.
Mwisho

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO