Thursday 11 April 2013

WAFANYABIASHARA SOKONI MAZESE SONGEA WALALAMIKIA UCHAFU KWENYE MADAMPO.

 Wachuuzi wa vitunguu ambao hawakutaka kutaja majina yao katika eneo la soko kuu la Songea wakisubiri wateja wao.
..................................................................... 

Na Amon Mtega ,Songea
 
WAFANYABIASHARA wa soko la mazese ,A, na ,B, lililopo kata ya Misufini manispaa ya Songea mkoani Ruvuma wameulalamikia uongozi wa kata hiyo katika kitengo cha afya kwa kushindwa kuwasiliana na uongozi wa manispaa wa kitengo hicho ilikufanikisha kuondoa taka zilizofurika kwenye madampo yaliopo sokoni hapo na kusababisha usumbufu kwa wafanyabiashara hao kwa kuwepo na harufu kali.

 Wakiongea na mwandishi wetu wa demashonews kwa nyakati tofauti katika eneo la tukio hilo mmoja wa wafanyabiashara Jastin Robo alisema kuwa taka hizo zimerundikwa hapo kwa muda mrefu licha bila kuzolewa licha ya wao kuwajibika katika utoaji wa ushuru.

 Robo alisema kuwa madampo hayo tangu yawekwe taka hayazolewi na sasa kwa kipindi cha masika hii kumekuwa na hali mbaya kwa takataka hizo kutoa harufu kali pamoja na kuchuja maji machafu ambayo ni hatari kwa mripuko wa magonjwa hasa ya kipindu pindu.

 “Sisi tunaulalamikia uongozi wa kata hii hasa katika kitengo cha afya kwa kushindwa kulifuatilia suala hili katika ngazi ya manispaa ili waweze kutatua kero hii maana sisi wafanya biashara tunaumia kwa harufu chafu kama hiyo”alisema Robo.

 Naye mwanamama Happnes Hyera anayefanyabiashara katika soko hilo alisema kuwa atha wanayoipata katika biashara hiyo kutokana na dampo hilo  kufurika kwa taka ni kubwa sana maana hata ulaji wa chakula cha mchana wawapo kazini hapo unakuwa ni washida sana .

  “Mwandishi chakula cha mchana tunakula  hapahapa maana hatuwezi kuondoka kwenda mbali kuyapisha madampo haya kwa kuwa biashara zetu zipo hapa na wateja wakija wakiona hatupo hawawezi kufanya biashara “alisema Happnes.

 Kwa upande wake diwani wa kata hiyo Salum Mfamaji kwa tiketi ya CHADEMA alisema kuwa tatizo la ujaaji taka huo unatokana na manispaa hiyo kutokuwa na vitendea kazi vya kutosha maana kwa sasa magari ya kuzolea taka yapo mawili tuu na ambayo yanafanya zamu ya kuzunguka katika kata mbalimbali.za manispaa hiyo.

 Aidha aliwaomba wafanyabisha hao kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kwa kuwa manispaa tayari inashughulikia kuongeza vitendea kazi ili kufanikisha kukabiliana na changamoto hizo kwa kuwa uzalishaji taka umeongezeka .

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO