Monday 22 April 2013

Joseph Joseph Mkirikiti “ Kuwa na fikra pana ni kujijengea hazina ya leo na kesho”


 
 Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti 
Wanachama wa Shirika la Restless development wakiwa katika kongamano

Hawa ni wanachuo waliojitokeza katika kongamano la  Restless development
..........................................................................
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Songea Bw, Joseph Joseph Mkirikiti katika  kongamano la vijana  lililofanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha  St. Augustine tawi la songea,

Kongamano hilo liliandaliwa na Restless development shirika lisilo la kiserikali ambalo linalofanya kazi na vijana katika nchi 11 ulimwenguni, ufundisha vijana na jamii kwa ujumla kuhusu afya ya uzazi na makuzi, jinsia, stadi za maisha, elimu ya uraia, ujasiliamali na kuwajengea uwezo vijana waliopo ndani na nje ya shule. Lengo kubwa ni kuwaweka vijana katika mstari wa mbele katika kujiletea maendeleo.

Joseph Mkirikiti amesema kuwa vijana ni kundi muhimu na ndio chachu ya maendeleo katika nchi yoyote ile na hakuna nchi iliyoendelea bila ya kuwatumia vijana kwani ni kundi lenye nguvu na tajiri wa maarifa.
Hivyo  kuachana na tabia ya kujivunia ujana kanakwamba ujana ni wamilele badala yake waone kule wanakokwenda na  wajielekeze katika fikra pana sio fikra finyu,

" Lazima utambue ujana ni ndoto kwa sababu kila dakika unayoyafikiria ni machache sana utayaota,  ndoto zenu zisiwe kutafuta ukubwa bali ziwe za kuwatumikia wanyonge,Nchi yetu inatumia rasilimali nyingi kuwasomesha vijana ambao mwisho wa siku wanaishia mitaani bila kuwa na ajira zinazoeleweka wala kujiajiri wao wenyewe walio wengi wanaosoma kwa malengo yakuwa viongozi na wengine hubagua kazi na hata sehemu za kufanyia kazi ,tutumie vyanzo tulivyo navyo kuleta maendeleo”

Kongamano hili limewakuwakutanisha vijana kutoka katika vyuo mbalimbali na shule za sekondari zilizopo manispaa ya Songea ili kuongeza jitihada katika kutengeneza sekta ya vijana iliyoimara.

 Kwa upande wake Bw. Lucian Sengesela ambaye ni mkufunzi wa chuo cha ualimu songea amesema ujana unakabiliwa na majukumu ya kuwa mzazi wa sasa na wa baadaye ikiwemo changamoto mbalimbali za maisha,maambukizi ya magonjwa hasa hatarishi kama vile ukimwi, changamoto za kimaadili, ukosefu wa ajira na kumiliki rasilimali.

“ ukosefu wa ajira kwa vijana unachangiwa na maadili ya tabia kwani vijana wengi kwa sasa hawana maadili hata maofosini wengi wao wako kisasa  zaidi  kwa kujiona wao ni wasomi, kubagua kazi  kwa kujiona wao ni wasomi hawezi kufanya kazi ambazo haziendani na hadhi yao,  pia wengi wao pale wanapopangiwa kazi vijijini hukataa kuripoti sehemu ya kazi  

Nae Bw. Nicas Ngumba ambaye ni mratibu wa  Restless development amesma  wameona haja ya kuandaa kongamano la vijana ili kuweza kujadili utambuzi wa fursa za uzalishaji mali, ajira na kujiajiri kama msingi wa kutengeneza sekta ya vijana iliyo imara, pia tuweze kutizama mfumo wa elimu na hasa ule wa vyuo ili kuweza kuona uwaandae vipi vijana ili waweze kunufaika na fursa za uzalishaji mali ili waweze kujiajiri wao wenyewe.
  

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO