Monday 8 April 2013

TEMBO WAENDELEA KUTEKETEZWA MKOANI RUVUMA




 
  kamanda wa polisi Mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimek akizishika nyara za serikali hizo ambazo zimekamatwa(mikia ya tembo)
 
Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma katika wilaya ya Tunduru kijiji cha mbalikiwa kata ya ligunga tarafa ya matemanga linamshikiria kijana amabaye anafahamika kwa jina la Bakari Said mwenye umri wa miaka 17 ambaye ni mkazi wa eneo hilo kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali.
 Nyara za Serikali ambazo zimekamatwa(mikia kumi ya tembo)
 
Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Deusidedit Nsimeki ameyasema hay oleo mapema wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema jumla ya mikia ya Tembo 10 imekamatwa na askari ambao walikuwa doria katika eneo la mbalikiwa mnamo 5.4.2013 majira ya saa:7 usiku ambapo jumla ya idadi hiyo ya mikia ni sawa na idadi ya Tembo 10 waliouwawa na idadi ya meno ni 20 yenye jumla ya dola za kimarekani elfu 15.


Mtuhumiwa Bakari Said leo anafikishwa mahakamani kwa tuhuma ya kujihusisha na biashara haramu ya nyara za serikali ambapo taharifa ya tukio hilo la uhalifu zilipatikana kutoka kwa raia wema pia kamanda wa polisi aliwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano waho wa dhati hili kuweza kudhibiti kabisa huarifu huo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO