Saturday 10 August 2013

JESHI LA POLISI LATANGAZA DAU LA MILIONI 10 KWA MTU YEYOTE ATAKAYEWATAJA WATU WALIOWAMWAGIA TINDIKALI RAIA  WAWILI  WA UINGEREZA

 
Zanzibar, Tanzania — Kamanda wa Polisi, Kamishna Musa Ali Musa amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa Shilingi milioni 10/= kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kukamatwa kwa watu waliowashambulia mabinti wawili kutoka Londona, Uingereza,  Kirstie Trup na Katie Gee.

Mabinti hao walishambuliwa kwa tindikali usoni, kifuani na mikononi siku ya Jumatano walipokuwa njiani kuelekea kwenye chakula cha jioni.



.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO