Thursday 15 August 2013

SIKU YA PILI YA MAFUNZO YA INTERNET AND JOURNALISM NI VITENDO ZAIDI



        Wawezeshaji wa mafunzo hayo wa kwanza kushoto ni Sengiyumva Gasiliwa na Saimon Berege
         Shukran wa Jogoo fm wa kwanza kushoto, julius konala wa Radio maria na Ennes wa Jogoo fm
   Joyce Joliga mwandishi wa gazeti la mwanachi na Kassiani Nyandindi mwandishi wa habarikutoka Mbinga
                                     Emmanuel Msigwa mwandishi wa channel ten naye akifanya zoezi
  Mwenye red ni Oswald Ngonyani Mhariri mkuu wa printing peramiho na Friday Simbaya wakielekezana kwa vitendo namna ya kutafuta material katika mtandao
 Mwenye tai ni Ngaiwona Nkondora wa Radio Free Afrika  akipongezana na Juma Nyumayo baada ya kufanya vizuri katika mafunzo hayo
       Mwenye shati nyekundu ni Steven Augustino kutoka Tunduru na kassian Nyandindi wa Mbinga


Na Steven Augustino na Catherine Songea
 

WAANDISHI wa Habari Mkoani Ruvuma wameonywa kuamini habari kutoka
mitandao na kuzitumia kuhabarisha umma bila  kuzifanyia utafiti wa
kutosha katika internet na kutumia vyanzo vya kuaminika ikiwemo
kuwahoji wahusika kupata habari za ukweli ambazo zitakuwa na manufaa
kwa wasomaji.
 

 Hayo yameelezwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa namna ya
kuandika Habari kwa kutumia mitandao ya Internet na kutuma picha za
kihabari  Mtandaoni yanayoendeshwa katika Ukumbi wa Veta,Manispaa ya
Songea, Taasisi ya Vyombo vya habari kusini mwa Africa (Media
Institute Of Southern Africa) MISA TANZANIA.
 

Wanahabari hao pia wanafundishwa namna ya kufanya utafiti wa vyanzo
vya habari mbalimbali katika Internet na kufungua njia nyingine za
mawasiliano kama  ‘youtube’, Blogu na namna ya kuzitumia katika tasnia
ya kutengeneza na kutuma habari zikiwa na takwimu sahihi.
 


Awali akiongea katika ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku tatu, Afisa
Habari MISA -TANZANIA , Sengiyuva Gasiligwa,  alisema kuwa lengo la
mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kwenda na
wakati hasa katika teknolojia ya kimtandao.
 


Wanahabari hao pia wananolewa ili waweze kujua kwa undani maana ya
internet, ‘Worid Wide Web’ , ‘Computer’,  na matumizi yake kwa manufaa
ya maendeleo ya technolojia, uchumi, siaa na utamaduni na kujali
maadili
Gasiligwa alisema kuwa mafunzo hayo yanayo wahusisha Waandishi wa
Habari za Magazeti, Terevissin na Radio yanafanyika kwa ushirikiano
MISATAN na shirika la VIKES  toka Finland na kwamba kwa kuanzia
mafunzo hayo yalifanyika Mkoani Pemba huku Zanzibar Tanzania Visiwani
na sasa Ruvuma na baadaye mkoani mwanza.
 

Nae mwezeshaji wa mafunzo hayo Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Tumaini
Iringa,  Saimon Berege,  pamoja na mambo mengine aliwataka Wanahabari
hao kuwa na ari ya kujiendeleza kielimu na kuwakaribisha kwenda kusoma
digrii ya pili (masters) Inayotolewa na chuo hicho.
 

Wakiongea kwa nyakati tofauti wanahabari hao pamoja na kuipongeza
taasisi hiyo kwa kuona umuhimu wa mafunzo hayo kwa waandishi wa habari
wamesema kuanzia sasa wataweza kufanya kazi za uandishi wa habari wa
kiuchambuzi kwa kuoanisha habari kutoka vyanzo vya mataifa mbalimbali,
kuandika habari kwa kutumia takwimu kutoka katika mitandao na kutumia
taarifa na hotuba zilizopita zilizotolewa na viongozi wa mataifa
mbalimbali duniani .
 

Aidha washiriki hao wameonyesha ushirikiano mkubwa katika uchambuzi wa
mada zilizotolewa na wameomba mafunzo kama hayo yatolewe mara nyingi
iwezekanavyo ili kuwakumbusha kuamsha ari ya waandishi.
 

Mwisho

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO