Saturday 10 August 2013




 10 Agosti 2013

Halmashauri ya manispaa ya Songea mkoani Ruvuma imetoa tamko juu ya vibanda vya biashara vya soko kuu la Songea kuwa mwisho wa kuchukua fomu na kujaza mikataba mipya mwisho tarehe 30/8/2013.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa manispaa ya Songea meya wa manispaa hiyo bwana Charles Mhagama  amesema atakayechelewa tarehe hiyo kuchukua fomu na kujaza mkataba mpya  atanyang’anywa kibanda na kupewa ambaye amechukua na kujaza fomu.

Tamko hilo limetolewa hivi karibuni baada ya wafanyabiashara kugoma kuchukua  na kujaza  mikataba mipya ambayo inaanza upya .
Halmashauri imeamua kupandisha pango la vibanda na huduma ya vyoo kutokana na kiwango wanacholipa wafanyabiashara hao kupitwa na wakati.

Wafanyabishsra hao awali walikuwa wanalipa shilingi elfu 40 hadi shilingi elfu 60 kwa sasa mikataba hiyo inaonyesha imeongeza pango hadi kufikia shilingi 130,000 kwa vyumba vya biashara hadi shilingi 200,000 kwa huduma za vyoo huku idadi ya vibanda ikiwa ni 130.

Katika maeneo ya katikati ya mji lilipo soko kuu la Songea wafanyabiashara wengine wanalipa hadi shilingi laki 4 kwa mwezi.

Manispaa ya Songea inakabiliwa na changamoto nyingi ambayo inahitaji fedha nyingi kukabiliana na kero hizo kama vile kushindwa kuzoa takaka  katika baadhi ya maeneo hata kwa mwaka mzima hususani eneo la majengo ,barabara nyingi za mji bado zina makorongo na vumbi, na huduma mbalimbali,

Changamoto nyingine ni kwamba mfuko wa mikopo wa serikali za mitaa unaidai manispaa hiyo zaidi ya shilingi milioni 126 hali inayoifanya manispaa hiyo kushindwa kukopa tena kutoka katika mfuko huo ili kujenga standi kuu ya mabasi na kuboresha huduma nyingine.

Hiyo ni taarifa kutoka uongozi wa manispaa na wameuomba umoja wa wafanyabiashara kutokuwa wachochezi kati ya manispaa na wafanyabiashara.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO