Monday 12 August 2013

 Na Amon Mtega,
        Namtumbo.
WATOTO wa nne wa Familia moja wa kijiji cha Ligunga kata ya Lusewa tarafa ya Sasawala wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma   wamefariki dunia na wengine 12 wamelazwa katika Hospitali ya mkoani humo na katika kituo cha Afya cha Lusewa kwa madai ya kula chakula kilicho kuwa kimewekwa sumu.
 
  Akiongea na waandishi wa habari katibu tarafa wa Sasawala Fred Maliyao alisema kuwa wanafamilia hao walikula vyakula vya karibu aina tatu na walikuwa 19 ambapo chakula kingine kilisadikika kuwa kilikuwa na sumu ambayo iliweza kuwazuru na kusababisha vifo hivyo.
 
  Maliyao alifafanua kuwa katika siku ya sikukuu ya IDD wanafamilia hao walikula chakula ugari kwa mboga ya samaki ,mbonga ya majani aina ya chaina na utumbo wa kuku ambao usadikika ulikuwa umechemshiwa mchuzi wa samaki huku wengine walikula ugali kwa mboga ya mbaazi ,utumbo wa kuku na mboga majani chaina.
 
  Alisema kuwa walikula chakula kwa baba yao mdogo na mkubwa  kwa zamu ambapo walikuwa wakiifurahia sikukuu ya IDD kwa familia hiyo kutembeleana na kufarijiana kwa sikukuu.
 
  Kwa upande wake mwanafamilia Bilahi Mumba alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 9 mwaka huu majira ya saa 5 hadi saa sita mchana baada ya watoto hao kula chakula kwa Baba yao mdogo Mumba ambaye anadai kuwa alinunua samaki hao kwa mtu mmoja katika eneo la Lusewa kwa bei ya shilingi 1500.
 
     “Nasisi tunashangaa tuliona muda mfupi baada ya kula chakula hicho walianza kuanguka na wengine kutapika huku tukijitahidi kuokoa maisha ya watoto hao lakini wanne wameweza kufariki na wengine tuliwakimbiza kituo cha afya cha Lusewa.
 
     Mumba aliiwataja watoto hao waliyokufa kuwa ni Zidane Mumba[2.5] Tazamio Mumba [9] Selemani Mumba [7] na Zahara Mumba [2] na kuwa wote ni wafamilia moja.
 
      Naye muuguzi wa kituo cha afya za Lusewa Edrisa Ndauka alisema kuwa walipokelewa wagonjwa 16 katika kituo hapo na wanne walifariki watano walikimbizwa hospitali ya mkoa Songea na kuwa wengine walibaki kituoni hapo.
 
         Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Namtumbo mkoani humo Abdula Lutavi ambaye naye alienda kushuhudia tukio hilo alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa kwa kuwa waliyoathirika ni watoto wa familia moja.
 
           Lutavi alisema licha ya watalamu kuchukua matapishi na mabaki ya vyakula hivyo kwa kwenda kuvipima lakini taarifa za awali zinaonyesha kuwa sumu iliwekwa kwenye samaki  maana wote waliyo gusa samaki au mchuzi wake wamepata athari.
 
    Mkuu huyo ametoa onyo  kwa baadhi ya watu wakijiji hicho  ambao huvua samaki kwa kutumia sumu mbalimbali zikiwemo za zao la Tumbaku kwa ajili ya kujipatia kitoweyo ,sasa waache mchezo huo badala yake watumie ndowano na nyavu.
 
       Kamanda wa polisi mkoani Ruvuma Deusdedit Nsimeki amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wanamshikilia mtu mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Salumu kwa mahojiano zaidi kuhusiana na tukio hilo.
 
                 MWISHO.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO