Thursday 18 July 2013

JAMANI SALON RAHA



kweli nimeamini ya kwamba salon za kike zinamambo jumamosi niliingia salon moja mitaa ya uhindini ndani mule kulikuwa na wateja wengine wengi tu wakitengeneza nywele zao na kucha, mara wakaingia wadada wawili ni wasichana tu wenye umri kama miaka 25-28 sasa wakiwa salon wanatengeneza kucha kuna dada mmoja akaanzisha story ya kuhusu mapenzi na jinsi gani anavyofurahia mapenzi anayopewa na mpenzi wake

pembeni ya huyo dada kulikuwa na mama mmoja yeye alikuwa anafanya steaming ya nywele wote tulikuwa tunasikiliza story tukicheka na kuchangia panapotakiwa, sasa cha kushangaza kati ya wale wadada walioingia wawili mmoja akaanza kutoa story ya bwana yake jinsi anavyompenda yani hajawahi kuona mtu kama yeye

isitoshe huyo dada akawa anajitamba kwamba mwanaume kampangia nyumba, anampa hela ya matumizi, kila anachotaka anapewa, kamnunulia gari na sasa hivi yule mwnanaume anamjengea huyo msichana nyumba pande za Ruhuwiko

yule msichana akiendelea kutupa story ya kuhusu huyo mwanaume wake yule mama mtu mzima akamuuliza huyo mwanaume wako ameoa? ama ni mwanaume mwenye mmpango wa kukuoa? yule dada akamjibu bado hawajaongelea hayo mammbo ila tu yule dada ni mjamzito na mimba ni ya yule kaka, ameona ampe zawadi ya mtoto kwa yote mazuri aliyemtendea..

watu wakazidi kuchokonoa story, wakamuuliza sasa huyo mwanaume wako anafanya kazi ama ni mfanya biashara yule dada akaanza kumwaga manyanga na kusema yule mwanaume anapofanya kazi, jinsi alivyokuwa mcheshi, na anaendesha gari na mpaka namba na aina ya gari akaitaja na kumalizia na kusema yani nipo tayari kwa kufanya lolote kwa mtu atakaye nichukulia mwanaume huyu..

JAMANI, JAMANI, JAMANI kweli nimeamini siku za mwizi ni forty, kumbe mwanaume wa yule dada ndio mume wa yule mama mtu mzima aliyekuwa pale saloni anafanya steaming nywele yula mama aliposikia mpaka namba ya gari lake limetajwa alicho kifanya ni alitoka kwenye steamer alimpiga yule mwanamke, jamani yule dada alipigwa

tukashangaa yule mama akifanya hivyo mara akasema "wewe nilikuwa nakutafuta siku nyingi sana" kumbe yule mama alishajuwa mume wake anahawara nje, alisha kuta simu akipigiwa mara nyingi sana yule mwanamke na message nyingi sana akituma na kutumiwa yule dada ila tu yule mama hakupata nafasi nzuri ya kumtafuta mpaka Mungu alipowakutanisha salon siku hiyo

yule mama akampigia mumewake simu amfwate ile salon alipo kwani walikuwa wanakaa jirani, makusudi tu ili amuone mume wanke angefanyaje kumuona yule hawara pale akiwa amepigwa basi yule baba kufika tu pale salon alivyomuona yule mke wake na hawara akadondoka na kuzimia...

sikutaka kufwatilia zaidi baadada ya mume kuanguka ila nikipata hiyo story ilivyokuwa baada ya pale nitakuja kuiandika tena, maana nitaenda tena ile salon

kweli nimeamini za mwizi zikifika zimefika...


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO