Sunday 7 July 2013

RAIS JAKAYA KIKWETE AFUNGUA MTANANGE WA SIMBA NA YANGA KWA WABUNGE

Rais Kikwete katika picha ya pamoja na Eric Shigongo, Waziri Fenella Mukangara, marefarii na manahodha wa Simba na Yanga.
Vikosi vya Simba na Yanga.
JK akipuliza kipenga.
Mtanange ukiendelea.
Score board ilisomeka hivi.
Mashabiki.


Sehemu ya nyomi ikilipuka kwa burudani.


Rais Kikwete.
Aidha, amesema kuwa shabaha ya tamasha hilo ni kuamsha upya imani ya Watanzania kwa nchi yao. Kuwafanya wawe wazalendo na kila mmoja kujiona analo jukumu la kufanya, kuhakikisha Tanzania yetu inapiga hatua.

“Mbali na Rais Kikwete, wengine watakaotoa neno la matumaini siku hiyo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, Eric Shigongo.
Zitto Kabwe.
“Wengine ni Mwenyekiti wa Taasisi ya East Africa Speakers Bureau Limited (EASB), Paul Mashauri, mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali, James Mwang’amba na mwanamitindo, Jokate Mwegelo.

“Wote hao, kila mmoja atakuwa na fursa ya kufikisha Neno la Matumaini ili kila atakayehudhuria Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, aondoke akiwa mpya, akiwa na matumaini mapya kwa taifa lake na maisha yake kwa jumla,” alisema Mrisho.
Nape Nnauye.
Kwa upande wake Shigongo amesema kuwa udini, ukabila na kila aina ya ubaguzi, vitachimbiwa shimo na kuzikwa.

“Taifa linapita kwenye kipindi kigumu ambacho ni changamoto nzito. Unazungumzwa ufisadi, migomo imekuwa mingi, udini na ukabila vinapenyezwa kwa kasi, pamoja na aina zote za ubaguzi, hivi vyote tunapaswa kuvizika.

“Tuna makusudio ya kuwafanya Watanzania wajione wamoja licha ya tofauti za kiitikadi zilizopo. Mahitaji yetu ni kupaza sauti kuwa kila mtu yupo huru kusimamia anachokiamini lakini linapokuja suala la umoja wa kitaifa, tofauti zote zinapaswa kuwekwa kando,” alisema Shigongo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO