Wednesday 10 July 2013

NAWATAKIA WAISLAMU WOTE RAMADHANI KARIMU

RAMADHAN‬ KARIM

Uzuri wa Ramadhani si tambi kwa iliki
     bali ni kusoma Qur-an kwa wingi.

Wala si uji kwa ndizi
bali ni kumuomba MOLA atuhifadhi.


                                                                                             

                                                      Tena si chapati kwa mchuzi


bali ni kuacha yote ya kipuuzi.

Na wala si juisi kwa sambusa za nyama
bali ni kuomba istighfar kwa Maulana.

Pia wala si daku la wali wa nazi kwa jodari
=bali ni tahajudi kwa wingi.


"MOLA AWAFIKISHE KUUDIRIKI MWEZI WA
RAMADHANI NA KUPATA FADHILA ZAKE".


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO