Thursday 11 July 2013

JENISTER MHAGAMA AWATAKA WANANCHI KUKATAA KUSHABIKIA SIASA ZA CHUKI



Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania JENISTER MHAGAMA amewasihi wananchi wa SONGEA kukataa kushabikia siasa za chuki zinazopandikizwa na baadhi ya wanasiasa wanaowachonganisha wananchi na serikali kwa madai kuwa serikali haiwajali watu wake.


JENISTER MHAGAMA ambaye pia ni mbunge wa jimbo la PERAMIHO Mkoani RUVUMA ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kufungua kata mpya ya Kichama ya MUUNGANO na kukagua ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha KILAGANO

pia wananchi wa Vijiji vya LUGAGALA na MUUNGANO ZOMBA vinavyounda matawi manane ya Chama cha Mapinduzi CCMwamefanya maandamano yamefanyika katika Kijiji cha LUGAGALA ambako Mwenyekiti wa Bunge JENISTER MHAGAMA ambaye ni Mbunge wa Jimbo la PERAMIHO, amezindua kata ya Kichama Itakayoitwa MUUNGANO ikiwa ni moja kati ya kata tano za Kichama zilizoanzishwa Songea Vijijini


Pamoja na shughuli hii ya Kufungua kata Mpya ya Kichama, JENISTER MHAGAMA pia alikua na shughuli nyingine ya kukagua Jengo la Zahanati ya Kijiji cha LUGAGALA likiwa ni jingo mojawapo kati ya Majengo sita ambayo wakati wa Mvua ilimlazimu kutafuta fedha kwa dharula kwa ajili ya kuyanusuru yasianguke, juhudi ambazo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya SONGEA RAJAB MTIULA amekiri kuwa zimeokoa jahazi

Ukiachilia mbali miradi hii ya Ujenzi wa Zahanati, JENISTER MHAGAMA ametumia Mkutano wake na wananchi kuwasihi wasikubali kushabikia siasa zinazopandikiza chuki na kulivuruga taifa na kwa Siku zote wazungumze ajenda ya Maendeleo na jinsi ya kupambana na umasikini kwa kushirikiana na serikali yao

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO