Wednesday 10 July 2013

JK AHUTUBIA MIAKA 50 YA JKT ASEMA CHANGAMOTO BADO ZIPO NYINGI


Mheshimi wa Shamsi Vuai Nahodha (Mb), Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa;
Mheshimiwa Gril Haskel, Balozi wa Israel;
Meja Jenerali Raphael Muhuga,Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa,
Makamanda, Wapiganaji na Vijana;
Wageni Waalikwa;
Ndugu Wananchi;
Mabibi na Mabwana;

Pongezi

Nakushukuru sana Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Raphael Muhuga kwa kunishirikisha kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhai wa Jeshi la Kujenga Taifa.

Nawapongeza sana kwa maandalizi mazuri ya sherehe hizi ambazo hakika zimefana sana. 
 Gwaride lilikuwa zuri na tumeburudika vya kutosha kutoka vikundi vya ngoma, ngonjera na nyimbo.

Kwa niaba yangu, ya Serikali na ya Watanzania wote nawapongeza kwa dhati Maafisa Wakuu, Maafisa Wadogo, wapiganaji na vijana wa JKT popote pale walipo kwa kusherehekea Jubilei ya Dhahabu ya uhai wa JKT.  Mnastahili kuwa na furaha na kusherehekea kama tulivyoshuhudia sote.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO