Sunday 28 July 2013

MDAU SIMALENGA WA CLOUDS FM AKUBALI YAISHE,AFUNGA NDOA NA NEEMA INANA .


Kambi ya Wasanii wa Filamu na Maigizo pamoja na Kambi ya Wanahabari Makapela Tanzania imepata pigo kubwa baada ya Mwanachama wake Nguli, Simon Simalenga kuamua kuiaga kambi hiyo na kuingia rasmi katika Kambi Tawala ya Wanandoa baada ya kufunga Ndoa na Bi. Neema Inana.

Wawili hao wameamua kuingia kambi hiyo ya Upinzani katika mahusiano leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mwokozi Sinza jijini Dar es Salaam na baadae katika tafrija kubwa inayofanyika usiku huu wa Julai 27, 2013 katika ukumbi qa Grande Hall uliopo ndani ya Hoteli ya Picolo Beach Mbezi. 


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO