Saturday 22 December 2012

CHAMA CHA AKIBA MIKOPO CHA WATUMISHI WA MANISPAA YA SONGEA KINA KISIA KUKUSANYA JUMLA YA TSH.600,000,000/=TOKA KATIKA VYANZO VYAKE VYA NDANI.


 Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU
Viongozi wa chama cha akiba na mikopo  cha watumishi wa manispaa ya songea mkoani Ruvuma wametakiwa  kuongeza kiwango cha kutoa  mikopo  kwa wanachama wake ili waweze kujiimarisha katika maisha yao
 Baadhi ya wanachama wa sacco's wakiwa katika maandamano
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma said mwambungu ameyasema hayo wakati akifungua mkutano mkuu wa 20 wa chama cha akiba na mikopo cha watumishi wa manispaa ya songea iliyofanyika katika ukumbi wa songea club.
wanachama wa sacco's manispaa ya songea
Amesema mikopo  waliokopeshwa wanachama  kwa ajili ya ujenzi  wa nyumba ni midogo ukilinganisha na gharama za vifaa vya ujenzi.hivyo wanachama wanaweza kujenga nyumba zilizo chini ya kiwango.
 Mea wa mji bwana Chales Mhagama
Pia  Viongozi wa chama cha akiba na mikopo cha watumishi wa manispaa ya songea mkoani Ruvuma wametakiwa kuendeleza utamaduni wa kuwa waaminifu katika kutunza mali na fedha za wanachama wao.
 Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkilikiti
 Akisoma risala ya mkutano mkuu wa 20 wa chama hicho mwenyekiti wa chama bwana Sky mpange amesema chama kimejipanga kuongeza mikopo ya ujenzi wa nyumba kutoka shilingi milioni nane hadi milioni kumi na mbili.
 Mwenyekiti wa chama bwana Sky Mpange
Mpaka sasa chama kina jumla ya akiba za wanachama zaidi ya  shilingi milioni miatatu na laki tisa, na kwa mwaka huu tayarikimekopesha wanachama wake zaidi ya shilingi milioni miatatu na laki nane.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO