Wednesday 26 December 2012

Mh.Filikunjombe (MB) Atembelea Hospitali Siku Ya Krismass

 Mbunge  wa  jimbo la Ludewa mkoani Njombe akiangua  kilio wakati akimsikiliza mtoto Diana  Haule (11) mkazi wa  Shauri moyo  wilaya ya Ludewa ambae amelazwa katika wodi namba  6 akitibiwa majeraha ya moto ambayo ameyapata baada ya  kuangukia motoni  kutokana na ugonjwa wa kifafa unaomsumbua
 Mbunge  Filikunjombe akitazama  mikoni ya mtoto Diana ambayo imeungua kwa moto kushoto ni mama mzazi wa mtoto huyo


Mbunge  wa  jimbo la Ludewa na familia  yake  wakiwajulia hali  wagonjwa kama ilivyoutaratibu  wake wa kila sikukuu kula na  wagonjwa wa zanahati na Hospitali mbali mbali  jimboni mwake .


Mbunge  wa  jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe leo amejikuta  akibubujikwa na machozi baada ya  kutembelea  wodi la majeraha ya moto katika Hositali ya Misheni Rugalawa na kukutana na mtoto Diana Haule (11) mkazi  wa Shaurimoyo ambae ameungua kwa moto mwili wake na kuimbiwa wimbo maalum uliomfanya  kutokwa na machozi.

Mbunge  huyo akiwa na familia  yake ya   mke  na watoto  wawili pamoja na viongozi  wa CCM  wilaya ya Ludewa aliofika katika wodi namba  6 ambalo mtoto  huyo amelazwa aliokelewa kwa  wimbo maalum kutoka kwa mtoto  huyo ambao  ulikuwa  ukimsifia mbunge  huyo na wakati akiusikiliza na kumtazama mtoto huyo mbunge huyo alianza kutokwa na machozi na kulazimika  kuwaomba  watu  ambao alikuwa ameongozana nao  kutoka nje ya  chumba hicho na kumuacha yeye na mtoto  huyo na watu  wachache.

katika  wimbo  huo mtoto  huyo alikuwa akieleza  jinsi ambavyo ameshindwa  kuendelea na masomo  kutokana na tatizo na ugonjwa wa  kifafa  linalomsumbua na  Pamoja na kumpongeza mbunge kwa  kufika kumjulia ari.

Kutokana na wimbo  huo mbunge Filikunjombe alijikuta akiinamisha  kichwa   chini na kuanza  kutokwa na machozi huku akiendelea  kumsikiliza mtoto  huyo akiendelea  kuimba.

Hata  hivyo mbali ya  kueleza  kusikitishwa na tatizo la mtoto  huyo bado mbunge  huyo aliahidi  kuendelea  kumsaidia mtoto  huyo ikiwa ni Pamoja na  kuisaidia  Hositali  hiyo  zaidi .

Mtoto  huyo anadaiwa  kuungua kwa moto toka mwezi  wa 9 mwaka  huu  baada ya  kuangukia motoni wakati akiwa na mamake mdogo jikoni akiendelea  kuandaa chakula .

Wakati huo  huo  mbunge  Filikunjombe amekabidhi misaada mbali mbali katika  Hospitali  hiyo yakiwemo mashuka kwa wagonjwa  wodi  zaidi ya 80 na kandambili pamoja na  kutoka msaada wa chakula  vyote  vikiwa na thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 2 


 Chanzo cha habari  http://www.mjengwablog.com/

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO