Monday 17 December 2012

Madhehebu Ya Dini Yatakiwa Kusaidia Makundi Yasiojiweza

 Mchungaji Shadrack Langu (katikati), wa kanisa la KKKT Amani akiwa na baadhi ya watoto na kikundi cha VICOBA baada ya kukabidhi
 Katibu VICOBA kanisa KKKT, Usharika Amani, Singida mjini Mwl Anna Abdalah  akikabidhi mafuta ya kula, ikiwa ni sehemu ya msaada
Na: Elisante John-Singida
KANISA la KKKT-Dayosisi ya kati Usharika Amani Singida mjini, umetoa wito kwa madhehebu ya dini kusaidia makundi maalumu yasiyojiweza ikiwemo watoto wanaoishi mazingira hatarishi.
Wito huo umetolewa na Mchungaji wa usharika huo, Shadrack Langu, wakati wa makabidhiano ya msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwa kituo cha Malezi, Kititimo mjini Singida.
A u, ili kujemesema utoaji wa misaada hiyo kwa makundi yasiyojiweza, itasaidia kuijenga moyo wa upendo baina yao.
Msaada huo wa kibinadamu uneotolewa na kikundi cha VICOBA, chini ya kanisa hilo, kwa ajili ya kituo hicho, chenye jumla ya watoto 40.
Mchungaji Langu amesema moja ya majukumu ya kanisa ni kuia jamii, hususani makundi yasiyojiweza ili kuwajenga kimwili na kiroho baadaye wamudu maisha yao.
“Kazi ya kanisa ni kuhakikisha mwanadamu anakombolewa katika maisha yake…ndiyo maana hata wamisionari walipokuja kwetu, walipojenga shule, walijenga pia zahanati na hospitali ili kusaidia jamii kimwili,”alisema mchungaji Langu.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi, katibu wa VICOBA –KKKT Amani, Mwalimu Anna Abdalah aliwaasa watoto hao kuondokana na huzuni badala yake wajione wapo sawa na watoto wanaokula, kulala na kuishi na sehemu nzuri wakiwa na wazazi wao.
Kwa upande wake mwangalizi wa kituo hicho anayetumia maisha yake kuishi na kuwahudumia watoto hao, Ali Makala alishukuru msaada huo na kuiomba jamii kuiga mfano wa akina mama wa VICOBA kutoka usharika wa Amani katika kusaidia kituo hicho.
Msaada huo unaojumuisha unga wa sembe kilo 150, mchele kilo 100, mafuta ya kula, sabuni, maharage, mafuta ya kupaka, dawa ya meno, kalamu, daftari, juisi, biskuti, miswaki na dawa ya kuulia kunguni, una thamani ya zaidi ya Sh. Milioni 1.1.

Chanzo  Mjengwahabari
 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO