Monday 17 December 2012

NMB FAMILY DAY NAMTUMBO BRANCH NI BALAAH

Meneja huduma kwa wateja Benki ya Nmb tawi la Namtumbo bwn:Mustapha Njovu kushoto aliye simama na kulia aliye kaa ni meneja wa Benki ya Nmb tawi la Namtumbo Bwn: Mwinyi.


Benki Nmb tawi la Namtumbo lafanya sherehe ya family day katika hoteliy ya Hertage Cotage iliyopo mjini songea ,hii ni sherehe ambayo ufanyika kila ifikapo disemba 16 ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni play to win
 
Familia mbalimbali za wafanya kazi wa Nmb tawi la Namtumbo zilijumuika pamoja kusherekea siku hiyo kukiwa kumeambatana na burudani za aina mbalimbali kama vile kuvutana  kamba,kukimbia ndani ya magunia,kukimbiza kuku,kucheza mpira wa miguu kwa akina Baba na mpira wa pete kwa akina Mama pamoja na mpira wa wavu(vollebally) na ikifuatiwa na burudani ya muziki ambapo familia zote zilijumuika kwa pamoja
Meneja wa huduma kwa wateja na meneja wa benki ya Nmb tawi la Namtumbo
Meneja wa benki ya Nmb Namtumbo Branch
Bwn:Mustapha Njovu akitafakari
Manager wa Nmb bank Namtumbo Branch bwn:,Mwinyi akijianda katika zoezi la kuvutana kamba na mmoja kati ya wafanyakazi wa benki hiyo ambaye ni  Bibi Oresta
Bibi Oresta akitafakali ni njia gani aitumie kumshinda meneja wake
Na huu ndio mpambano wa kwanza katika zoezi la kuvutana kamba
Jamaa alishinda lakini shughuli ilikuwa pevu kumvuta dada Oresta
Mmoja kati ya wafanyakazi wa Benki hiyo Ezekiel akijichukulia ushindi kwa tabu sana baada ya kumvuta kijana machachari
Hatimae zoezi la kushindana kukimbia ndani ya magunia likaanza kwa upande wa wakina mama.
Nazamu ya akina baba ikafuatiwa baada ya akina mama kumaliza zamu yao.
Jamaa alishinda kuku baada ya kutumia taimingi za kipekee kukamata kuku huyo Bw:Mustapha Njovu
Mtoto Fatima Shaban akitokelezea
Maongezi nae hakuwa nyuma siku hiyo

Na hii ni picha ya pamoja ya familia zilizo hudhulia sherehe hiyo

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO