Saturday 22 December 2012

KUTOKANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MAISHA YA WAKAZI WA MANISPAA YA SONGEA YAPO KATIKA CHANGAMOTO KUBWA

Wazazi wanatakiwa kuwaangalia kwa karibu watoto wao katika kipindi hiki cha masika .
 Ni Baadhi ya Watoto wakichezea maji machafu ambayo yanatililika kutoka maeneo mbalimbali
 Kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha katika Manispaa ya Songea Baadhi ya mashimo ya vyoo ya zibuka na kutoa maji machafu yakiwa yameambatana na maji ya mvua ambapo watoto wadogo wamefanya maji hayo ndio mchezo wao mkubwa katika michezo yao ya kuchezea maji bila kujali machafu au laa.
Baadhi ya wafanya biashara ndogondogo ususani wauza mboga wamekuwa wakitumia maji ya mito kuoshea biashara zao ambazo ni za mboga na kuhatarisha maisha ya wakazi wa manispaa kiafya.
 
 Muuza mboga za majani akitoka mtoni kuosha mboga zake kisha kuzikpeleka katika soko la kuuzia
 Aidha baadhi ya maeneo ya barabara yameharibika na mvua hizo na  madaraja mbalimbali yamebomoka kutokana na maji kuwa mengi sana hivyo kusababisha foleni ya magari ambayo yanapita katika eneo hilo.
 barabara ya bombambili,matarawe ilivyoharibiwa na mvua

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO