Sunday 23 December 2012

MKUU WA MKOA WA RUVUMA BW. SAID MWAMBUNGU AWAPONGEZA WAANDISHI WA HABARI WA MKOA WA RUVUMA KWA KUANZISHA RADIO YA WAANDISHI WA HABARI


 Nimoja ya Radio iliyotolewa na UTPC
 Camera aina ya Canon iliyotolewa na UTPC

 Katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani RUVUMA ANDREW
CHATWANGA akimuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Saidi Thabiti Mwambungu Studio

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU amewapongeza  waandishi wa
habari wa mkoa wa Ruvuma kwa kuanzisha radio ya waandishi wa habari
ambayo itasaidia kuleta maendeleo ya mkoa.

Akikabidhi vifaa vilivyotolewa na muungano wa vyama vya waandishi wa
habari nchini UTPC  kwa waandishi wa habari hao mkuu huyo wa mkoa
saidi mwambungu amesema vifaa hivyo Vimetolewa katika muda muafaka
kwakuwa vingine  vitatumika  katika matangazo ya radio ambayo iko
mbioni kuanzishwa.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na photocopy mashine, desktop computer,
deskopt monitor, printer,laptop, universal power supply (ups) Binding
machine, lamination machine, digital tape, Dvd player, Projecta, Radio Sony na TV set

utokana na umuhimu wa vifaa hivyo mkuu wa mkoa wa Ruvuma amewataka
waandishi wa habari kuweka utaratibu wa namna ya kuvitmia ili vitunzwe
vizuri.
Aidha amewatia moyo wa kuendelea na mipango ya kufungua kituo cha
radio ambayo itawaletea ajira kwa waandishi ambao bado hawapata ajira.

Naye katibu wa chama cha waandishi wa habari mkoani RUVUMA ANDREW
CHATWANGA ameseam tayari waandishi wamejipanga kutumia vifaa hivyo kwa
utaratibu maalumu na kuhakikisha vinatunzwa vizuri.

Akizungumzia suala la uanzishwaji wa radio ya waandishi wa habari
mkoani Ruvuma chatwanga amesema mipango ya uanzishwaji radio
inaendelea vizuri, na sasa kituo cha radio kinaendelea kutengenezwa.

Rashid Ngelangela ni mmoja kati ya waandishi wa habari kutoka manispaa
ya songea akitoa shukrani kwa mkuu wa mkoa amesema waandishi wa mkoa
wa Ruvuma watazingatia yote aliwaasa.

Naye makamu mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Ruvuma
LATECIA NYONI  aliwashukuru waandishi kwa umoja wanaoendelea
kuuonyesha katika kutekeleza kazi zao

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO