Monday 24 December 2012

WAKAZI WA MANISPAA YA SONGEA MKOANI RUVUMA WAMEFURAHIA KUTOPANDA KWA BEI ZA VYAKULA KATIKA KIPINDI HIKI CHA KUELEKEA SIKUKUU YA X – MASS NA MWAKA MPYA


Wakazi wa Manispaa ya SONGEA Mkoani RUVUMA wamefurahia kutopanda kwa
bei za vyakula katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya X-Mass na Mwaka mpya, licha ya baadhi yao kudai bei kubwa ya nguo na mapato kidogo ya kilimo waliyoyapata msimu huu vimesababisha changamoto yakushindwa kukidhi mahitaji yao

Kwa upande wa Vyakula, imekua neema kwa wananchi safari hii. Vyakula hususani Mchele unaouzwa kwa kati ya shilingi 1600 hadi shilingi 2400 haujabadilika bei, Nyama nayo haijabadilika bei na hata wafanyabiashara wenyewe wanasema hawatapandisha bei msimu huu Nae Mkuu wa Masoko ya Manispaa ya SONGEA SALUMU HOMERA amewapongeza wafanyabiashara katika masoko yake kwa kutopandisha bei za vyakula msimu huu wa sikukuu

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO