Tuesday 1 January 2013

TUFAE YAPANIA KUMKOMBOA MTOTO WA KIKE KIELIMU


Na,Steven Augustino  Tunduru
 Wazazi na Walezi wameaswa kushirikiana na Serikali kusimamia na kufuatilia   kwa karibu mienendo na maendeleo ya Watoto wao hasa wa kike zikiwa ni juhudi za kuhakikisha  kuwa  watoto hao wanafanya  vizuri katika masomo yao na kujiletea maendeleo yao.
Wito huo umetolewa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru Bw.Chande Nalicho na Mtendaji wa Kata ya Muhuwesi Bw. Shaibu Ngoronje wakati akiongea katika mkutano wa Wadau wa elimu uliofanyika katika Kijiji cha Mhuwesi  ukiwa ni mwendelezo wa juhudi za Mradi  wa Usimamizi na Utetezi wa Haki ya Mtoto wa kike kupata elimu .

 Akifafanua taarifa hiyo Bw.Ngoronje alisema ili kufanikisha adhima hiyo serikali imejipanga kutoa elimu kwa kuwaomba wazazi pia walezi kujitoa kuchangia chakula  cha mchana kama kivutio ili kuwaongezea nguvu ya kusoma watoto hao katika masomo yao.

Katika utafiti huo uliofanyika katika Tarafa za Muhuwesi,Namasakata,Ligoma,Nandembo,Mlingoti Mashariki na  Mlingoti Magharibi zilibainisha kuwapo kwa kundi kubwa la watoto wa kike waliopata mimba pamoja na kikwazo cha uelewa mdogo wa jamii juu ya SERA ya Elimu,Haki ya mtoto wa kike kupata Elimu,Mila zilizopitwa na wakati.

Alisema Takwimu hizo zilifafanua kuwa katika kipindi cha Mwaka 2007-2010 jumla ya waliotarajiwa kuandikishwa shule ni watoto wa kike 17,386, walioandikishwa ni 14,692 ambao ni Sawa na asilimia 85.49%  na waliosajiliwa ni 13,411, na waliofanya mitihani wa kumaliza darasa la saba walikuwa 13,097 ambao ni sawa na asilimia 97.65%, huku kukiwa na anguko la watoto 314 ambao waliacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwemo kupata mimba wakiwa shuleni pamoja na utoro.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO