Wednesday 9 January 2013

rais shein azindua barabara

shein 31ce8
Na Ali Issa-Maelezo Zanzibar   9/1/2013
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ameuagiza uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano kuziwekea Mipaka maalum barabara zinazojengwa Zanzibar ili Wananchi waepuke kujenga pembezoni mwa barabara hizo.
Hayo ameyasema jana huko Bumbwini-Mfenisini wakati wa ufunguzi wa barabara hiyo ikiwani ni mwendelezo wa shamra shamra za kutimiza miaka 49 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Dkt. Shein amesema kwa kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kuepukana kuwalipa fidia Wananchi ambao wanatabia za kujenga katika maeneo ya barabara kwa kutarajia malipo pale nyumba zao zitakapobomolewa kufanya utanuzi wa barabara hizo.

 “Mnawachia watu wanajenga pembezoni mwa bara bara wakati mnawaona, mtu anaaza msingi, anainua tofali, anaezeka ,na anapiga palasta na nyinyi mnashuhudia,lazima iwekwe mipaka ya kuonesha eneo hili halipaswi kujengwa na atakae jenga avunjiwe .”alifahamisha Dkt.Sheini.
Alisisitiza kuwa babara ina mipaka yake maalum na kwamba mtu atakayebainika kujenga nyumba kwenye mipaka hiyo lazima ivunjwe kwani mtu huyo atakuwa anakwenada kinyume na taratibu za bara bara.

Dkt. Shein alitoa mfano wa barabara zilizojengwa nyumba pembezoni ambazo zinatarajiwa kutanuliwa siku za karibuni kuwa ni bara bara ya Magomeni-Kwerekwe na barabara ya Bububu kuelekea Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Alisema bara bara hizo ziliwekewa maeneo yake kwa ajili ya utanuzi siku za usoni lakini hakukuwa na mkakati wowote wa kulinda mipaka ya barabara hizo jambo ambalo liliwapelekea wananchi kupuuza sheria kwa kujenga nyumba.

Aidha Dkt. Shein aliwataka watendaji wa Wizara hiyo kuzitunza vyema Bara bara hizo alizozizindua pamoja na Madaraja manne ikiwa ni pamoja na kupanda miti pembezoni na kuepusha kuchomwa moto kwa kutumia matairi ili zisipoteze kiwango chake.

Nae Mwakilishi mkazi kutoka AFDB Bank Bi Toniya Kandiyero alisema kuwa Bank yao ipo mstari wa mbele kusaidia maendeleo ya Zanzibar katika miradi mbalimbali ambapo kwa upande wa Barabara imesaidia takribani Kilomita 83 katika maeneo ya Unguja na Pemba.
Bi Toniya alisema kwa sasa benki yake imejipanga kusaidia maeneo mengine mapya kama vile mazingira ya bahari na raslimali zake pamoja na shughuli zinazo fanywa baharini.

Bara bara ya Bumwini-Mfenisini imejengwa kwa kiwango cha lami na kampuni ya kizalendo ya MECCO ambayo inaurefu urefu wa kilomita 13.2 ikiwa ni msada wa fedha kutoka bank ya Afrika  AFDB.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO