Sunday 13 January 2013

MDAU WA ELIMU WILAYA YA SONGEA JABIRI KILIHAMA AMETOA MSAADA WA MIFUKO 50 YA SALUJI KWA AJILI YA KUSAIDIA UJENZI WA HOSTELI KWA SHULE SEKONDARI YA MAHANJE


Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Joseph Mkirikiti 

MDAU wa elimu wilaya ya Songea Jabir Kilahama ametoa msaada wa mifuko hamsini ya simenti kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa hosteli kwa shule ya sekondari ya mahanje iliyopo Madaba ili kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu wanafunzi kwenda shuleni hapo.

Akizungumza jana mara baada ya kukabidhi msaada huo ,Mkurugenzi wa Lutukira mixed Farm L.T.D Kilahama alisema ameguswa na matatizo ya ukosekanaji wa hosteli hivyo akaona naye anajukumu la kusaidia ujenzi huo hivyo ametoa msaada wa simenti mifuko 50 .

"Nimevutiwa kuchangia maendeleo ya elimu kwa wananchi wa wilaya ya songea kwani elimu ndiyo msingi wa masiha, nimetoa mifuko hamsini kwa ajili ya ujenzi wa hosteli ya wanafunzi wa shule ya sekondari mahanje,"alisema.

Akipokea msaada huo jana Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Joseph alimpongeza Kilahama kwa msaada alioutoa ambapo amewataka wadau wengine wenyeuwezo wajitokeze kusaidia maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo.

Amesema, bado wilaya inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya ujenzi wa mabweni, maabara za sayansi,nyumba za walimu, madarasa , matundu ya vyoo pamoja na ukosekanaji wa madawati.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO