Tuesday 8 January 2013

ASKARI WA MAGEREZA WAASWA KUFANYA KAZI ZA ZIAADA ILI KUINUA KIPATO CHAO

 Mkuu wa mkoa wa ruvuma SAID thabit MWAMBUNGU 
Hayo yamesemwa na   Mkuu wa mkoa wa Ruvuma SAID MWAMBUNGU wakati alipo tembelea katika ofisi za magereza zilizopo Mahenge Mjini Songea ambapo amewataka askari wa jeshi la magereza kujishughulisha na shughuli zingine za kiuchumi ilikuongeza kipato chao lakini wahakikishe hizo shughuli hazihasili,kudhuru au kuingilia maadili ya kazi zao.

Mkuu wa Magereza Mkoani Ruvuma ASP ALLY  A. KEREHEWA katika ripoti yake kwa Mkuu wa Mkoa alitanguliza shukrani zake za dhati kwa kutembelea magereza kwani kwa mala ya mwisho kwa viongozi kutembelea magereza kwa mkoa wa Ruvuma ilikuwa ni 27.9.2009.
Kwa mkoa wa Ruvuma unajumla ya watumishi 421,wafungwa 395 na mahabusu 321 ambapo kwa Mkoa wa Ruvuma unajumla ya magereza 6 ambayo ni gereza la  Kitai  lililopo wilayani Mbinga ambalo lilianzishwa mwaka 1969 na linajishughulisha na kilimo cha mahindi na ufugaji,gereza lingine ni la Songea Mjini lililo anzishwa mwaka 1948 na linajishughulisha na Usafi wa mazingira,kilimo ch a bustani na ujenzi na magereza mengine ni gereza la Tunduru,Mkwayu,Majimaji lililopo wilayani Tunduru na gereza lingine ni la mbinga.
Pia Askri wa magereza alichukuwa fursa hii kumueleza Mkuu wa mkoa kuhusiana na changamoto ambazo zinawakabiri kwa kiasi kikubwa ni pamoja na hustawi wa watumishi ni hafifu ikiwa pamoja nyumba ambazo wanaishi na ombilao kubwa kwa Mkuu wa Mkoa lilikuwa ni kupatiwa ofisi mpyaa ambayo inajitoshereza na hapo Bwana Said Thabit Mwambungu alihaidi mifuko 50 ya simenti kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO