Sunday 13 January 2013

JESHI LA ZIMAMOTO LATOA ELIMU YA KUKABILIANA NA JANGA LA MOTO SONGEA

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu 
Kamanda wa Jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoa wa Ruvuma Baraza Mvano
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bw. Said Thabiti Mwambungu akizima moto
Askari wa Jeshi la zimamoto

Jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani Ruvuma  limetoa elimu kwa wananchi juu ya kukabiliana na majanga ya moto katika sehemu za kazi, majumbani na mashambani. 

Kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoani hapa BARAZA MVANO amesema jeshi hili limelazimika kutoa elimu ya kukabiliana na majanga ya moto kwa kuwa wanachi wanapopatwa na mataizo ya kuunguliwa nyumba ama mali zao hawatoi taarifa kwa wakati.

Amesema jeshi hili lina majukumu mengi yakiwemo ya kuzima moto wenye madhara, kuokoa maisha ya watu na mali zao , kufanya ukaguzi wa kinga na tahadhari ya moto , kukusanya madhuhuli ya serikali na kutoa mafunzo ya kinga na taadhari.

Pia amesema jeshi hilo limejiwekea mikakati ya kuelimisha wananchi katika wilaya zote tano za mkoa wa Ruvuma namna ya kuzima moto ili kupunguza madhara ya moto na wananchi kuelewa majukumu ya jeshi hilo.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Bw.Said Thabiti Mwambungu akatumia nafasi hiyo kuwataka wale wote wenye tabia za kuchoma moto barabarani na kwenye makazi ya watu waache  mara moja. Kwani uchomaji wa moto ni uhalibifu  wa mazingira na usababisha madhara makubwa sana hivyo serikali haitawafumbia macho.

Pia amewaomba wananchi wawafichue wale wote wenye tabia hizo sababu wanawafahamu hivyo wasiwaogope kuwafichua ili kukomesha majanga haya ya moto

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO