Thursday 6 June 2013

Waziri mkuu Mhe. Pinda ashiriki Mkutano Mkuu wa Kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, jijini Arusha


IMG_0141
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Magesa Mlongo  akiwakaribisha Wajumbe kwenye  Mkutano Mkuu wa  Mwaka wa Kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, jijini humo. wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo. IMG_0154
Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe (Mb)  akihutubia wajumbe (hawapo  pichani) kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji  Vijijini, unaojadili utekelezaji wa kuwapatia IMG_0162
Waziri Mkuu Mizengo K. P. Pinda  akihutubia wajumbe (hawapo  pichani) wakati wa ufungunzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji  Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa kuwapatia wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo. IMG_0169
Wajumbe wakifuatilia hotuba ya Waziri Mkuu Mhe.  Mizengo K. P. Pinda  hayupo pichani wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji  Vijijini, Jijini Arusha unaojadili utekelezaji wa kuwapatia wananchi wa vijijini huduma ya maji kwa mwaka 2012/2013 na kuweka mikakati ya kukabiliana na changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji huo.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amefungua Mkutano Mkuu wa Kujadili Utekelezaji wa Miradi ya Maji Vijijini, jijini Arusha mwanzoni mwa wiki hii. Mkutano huu unalenga kujadili changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa programu katika mwaka 2012/2013 na namna ya kuzikabili changamoto hizo.

Akifungua mkutano huo, Waziri Mkuu aliagiza Halmashauri zote kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya maji kwa vijiji 10 na ujenzi wa miradi ya maji inayoleta matokeo ya haraka katika kipindi cha mwaka 2012/13 na 2013/14.

Waziri Mkuu alisisitiza kuwa mwelekeo na malengo ya mkutano huu uwe ni kujenga mkakati endelevu wa kutoa huduma ya maji kwa kuzingatia mahitaji ya kiuchumi na kijamii hususan wananchi walioko vijijini kwa lengo la kuwaondolea adha kubwa ya ukosefu wa maji.

“Hili linawezekana kama kila mmoja wenu anatimiza wajibu wake kwa bidii, maarifa, juhudi na nidhamu ya hali ya juu, nawakumbusha kuwa, jukumu mlilopewa na taifa ni kubwa na muhimu sana.” Alisema Waziri Mkuu.

Waziri wa Maji Prof. Jumanne Maghembe, akimkaribisha Waziri Mkuu kufungua Mkutano huo, aliwataka washiriki kutekeleza jukumu la kuwapatia wananchi washio vijiji huduma ya maji kwa kutumia fedha zinazotolewa kwa ajili ya kutekeleza miradi.

“Fedha tunazopewa ni za wananchi, na ni lazima tuweze kueleza kila shilingi iliyopokelewa imefanya kazi gani ikiwa ni sehemu ya uwajibikaji”. Alisisitiza Waziri Maghembe.

Mkutano huu umeanza tarehe 3 hadi tarehe 7 Juni 2013, na mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwa ni pamoja na yaliyojitokeza katika ufuatiliaji wa miradi ya maji nchini kwa mwaka 2012/2013, mpango wa utekelezaji wa miradi ya maji kwa mwaka 2013/2014.

Nyingine ni Utekelezaji wa Kampeini ya Kitaifa ya Usafi wa Mazingira, yaliyojitokeza wakati wa kupitia Mfumo wa Kiteknolojia wa Kutoa Taarifa (MIS), kila mkoa utatoa taarifa ya hali ya utekelezaji wa miradi ya maji kwenye vijiji na miradi mingine ya maji, mfumo wa ufuatiliaji wa kikanda na mapitio ya usanifu wa miradi ya maji.

Washiriki wa mkutano huu wanajadili namna ya kuongeza kasi ya Utekelezaji wa Mpango wa Mwaka 2013/2014 ikizingatiwa ni mwaka wa kwanza wa Utekelezaji wa Mpango Mpya wa Kuleta Matokeo ya Haraka Sasa (Big Result Now). Ambapo baada ya majadiliano washiriki wataingia mkataba wa kiutendaji (Performance Agreement) kati ya Halmashauri na Mkoa na kati ya Mkoa na OWM – TAMISEMI.

Mkataba huo utakuwa na majukumu ya kila mtekelezaji na hatua anayotakiwa kufikia katika kipindi cha mwaka 2013/2014 kwa kufuata viashiria vilivyowekwa kitaifa.

Mkutano huu unahudhuriwa na Waheshimiwa Wabunge, Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Wakurugenzi kutoka Wizara mbalimbali zinazoshirikiana na Wizara ya Maji, Wataalam wa maji kutoka Wizara ya Maji, Wataalam wa Maji kutoka Sekretarieti za Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini, na Wahandisi wa Maji kutoka Halmashauri. Pia, tumewashirikisha Wataalam kutoka katika sekta binafsi ambao tunashirikiana nao katika kufikisha huduma ya maji kwa wananchi waishio vijijini.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO