Monday 24 June 2013

POLISI RUVUMA WAKAMATA MENO 18 YA TEMBO

WATU WANNA WANATAFUTWA NA JESHI LA POLISI MKOANI RUVUMA BAADA YA KUTELEKEZA MENO YA TEMBO KUMI NA NANE KATIKA KIJIJI CHA MAJALA KATIKA WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA .

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI OFISINI KWAKE KAMANDA WA POLISI WA MKOA WA RUVUMA DEUSDEDITI NSIMEKI AMESEMA TAREHE 19.6.2013 MAJIRA YA SAA NNE USIKU ASKARI POLISI WA WILAYA YA TUNDURU WAKIONGOZWA NA MKUU WA UPELELEZI WILAYA YA TUNDURU NA WAKISHIRIKIANA NA MAAFISA WANYAMAPORI  WALIFANYA DORIA NA KWA PAMOJA KWA AJILI YA KUWAFUATILIA WATU WANAOSAFIRISHA NYARA HIZO KUTOKA KIJIJI CHA LIGUNGA KWENDA KIJIJI CHA MAJALA .

MNAMO TAREHE 20.6.MWAKA HUU MAJIRA YA SAA 3.00 USIKU NJE KIDOGO YA KIJIJI CHA MAJALA KATA YA NANDEMBO WILAYA YA TUNDURU MKOANI RUVUMA  ASKARI WALIWEZA KUONA WATU WANNE WANASUKUMA BAISKELI KUELEKEA KIJIJICHA MAJALA, WATU HAO BAADA YA KUONA MWANGA WA TAA ZA GARI LILIKUWA NA ASKARI POLISI NDIPO WALIPOLISHTUKIA NA KUTUPA BAISKELI ZAO NA KUKIMBIA.

BAISKELI HIZO ZILIKUWA ZIMEFUNGWA VIFURUSHI NA ASKARI WALIPOFIKA ENEO HILO WALIGUNDUA KUWA NI MENO YA TEMBO HIVYO WALIFANIKIWA KUKAMATA MENO YA TEMBO 18 YENYE UZITO WA KILOGRAM 84 NA THAMANI YA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 200 .

AIDHA KAMNDA WA POLISI WA MKOA WA RUVUMA AMETOA ONYO KWA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI HILO ILI KUFANIKISHA KUKAMATWA KWA WATU HAO.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO