Wednesday 5 June 2013

Mgogoro wa wachinjaji waibuka tena kwa kasi Songea

 Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akiongea kwa msisitizo ofisi juu ya mgogoro
ulijitokeza baina ya wachinja ng'ombe na wauzaji hapani ofisini kwake alipokuwa akiongea na waandishi wa habari
Aliyenyoosha kidole ni Issa Bakari  akionyesha banda lililobomolewa na  Afisa mifugo wa manispaa ya Songea

Hawa ni wachinjaji wa ng'ombe wakiwemo wauzaji wa ng'ombe wakiwa katika hali ya majonzi baada ya kuvunjiwa banda la kuhifadhia  ng'ombe kabla ya kuchinja
Waandishi wa habari wakimuoji Afisa mifugo mkoa wa Ruvuma Bw. Mwaiganju  aliyesimama katikati ni mwandishi wa habari wa ITV Bw. Nathan Mtega , anaefuata ni mwandishi wa habari wa radio Jogoo Millan  na alieshikilia kamera ni Demasho

Hawa ni baadhi ya ng'ombe ambao wapo uwanjani baada ya kuvunjwa banda
..........................................................

MGOGORO umeibuka baina ya wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe wa Manispaa ya Songea dhidi ya baadhi ya watumishi wa idara ya mifugo wa Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma ambao umesababisha wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe kuitisha mgomo usio na muda maalumu mpaka ufumbuzi   wa tatizo hilo ambalo walidai ni la muda mrefu upatikane.
 
Mgogoro huo ambao ulianza Juni 4 mwaka huu majira ya saa 12.30 jioni na kudumu mpaka majira ya saa 2 usiku mwenyekiti wa umoja wa wachinjaji wa  ng’ombe wa Mmkoa wa Ruvuma  Salum Mfamaji ambaye pia ni diwani wa kata ya Misufini  alipotangaza kusitisha huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo ambalo lilikuwa liliwataka wachinjaji na wauzaji wa ng’ombe kuondoka katika eneo hilo na kwenda kufanyia shughuli zao katika kata ya Tanga ambako wao walidai hakujaandaaliwa.
 
 Akizungumza kwa niaba ya wachinjaji Issa Bakari alisema kuwa wao kama wachinjaji hawajakaidi uamuzi wa Manispaa ya Songea kuhamia katika eneo hilo jipya lakini walishaomba eneo hilo lifanyiwe marekebisho muhimu ikiw ni pamoja na kuweka miundo mbinu muhimu  ikiwemo vyoo na maji kwa ajili ya usalama wa kiafya kwao na watu wengine watakaokwenda katika eneo hilo kwa ajili ya kupata huduma  hiyo muhimu.
 
 Alisema kuwa tangu kulipotokea mabadiliko ya watumishi katikas halmashauri ya Manispaa ya Songea na hasa katika idara ya mifugo kumeibuka na vitendo vya unyanyasaji kwa wachinjaji vinavyofanywa na baadhi ya watumishi wa idara hiyo ikiwa ni pamoja na kitendo cha kuamua kuvunja zizi la kuwafadhi ng’ombe kabla ya kuchinjwa kitendo ambacho kimefanywa bila kutolewa taarifa kwa wachinjaji na wao wameamua kusitisha huduma hiyo kwa jamii.
 
 Baada ya mjadala wa muda mrefu diwani wa kata Msamala eneo ambalo  machinjio yapo Sharif Mgwasa alipowaomba wachinjaji hao kuendelea kutoa huduma hiyo muhimu kwa jamii wakati uongozi ukiendelea na mazungumzo ya kutafua ufumbuzi wa tatizo hilo lililojitokeza ikiwa ni pamoja na kujua aliyeamuru kuvunjwa kwa zizi hilo bila kuzingatia utaratibu wa ushirikishwaji wa wachinjaji’wauzaji na  uongozi wa Manispaa hiyo.
 
Hata hivyo wachinjaji hao waliendeleakusisitiza kuwa hawako tayari kuendelea na huduma hiyo mpaka hapo ufumbuzi wa tatizo hilo utakapopatikana hali iliyoendelea mpaka Juni 4 mwaka huu majira ya saa 2 asubuhi walipoamua kuanza kuchinja ingawa ni ng’ombe wachache waliochinjwa kwa sababu ya sintofahamu hiyo iliyotokea huku eneo hilo la machinjio likitawaliwa na vurugu zilizosababisha askari polisi kufika eneo hilo na kutuliza ghasia hizo.
 
 Naye Mkuu wa wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumzia hali hiyo iliyojitokeza alisema kuwa hiyo imetokana na kutokwepo kwa ushirikishwaji wa pande zote zinazohusikia lakini pia suala la kuvunja zizi hilo haliafiki ni si utaratibu wa busara kwa sababu ni kitendo cha kihuni na hakipaswi kufumbiwa macho kwa sababu wachinjaji na wafugaji walipaswa kuandaliwa mazingira mapya ya kufanyia shughuli zao na suala la kuwahamisha lingefuata.
Hata hivyo ufumbuzi wa sintofahamu hiyo unatarajiwa kufikiwa kesho kwa kuzikutanisha pande zote kwenye ofisi ya Mstahiki Meya wa Manispaa ya Songea
Mwisho.
  VIA/www.demashonews.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO