Saturday 15 June 2013

Habari zilizotufikia hivi punde kutoka chanzo chetu cha habari kutoka jijini Arusha zinasema kwamba kitu kinachosadikika kuwa ni bomu limelipuka kwenye mkutano wa chadema jijini Arusha limeua watu wawili na kujeruhi wengine. 
 
Na gari la hospitali limevunjwa vunjwa vioo na watu wanaosadikika kuwa na  hasira kali baada ya kuchelewa kuwachukua majeruhi hospitalini wakati hali zao ni mbaya. Na hivi sasa watu wanatumia magari yao binafsi kuwapeleka majeruhi hospitalini . Napia kamanda mkuu wa mkuu wa mkoa wa Arusha yuko kwenye eneo la tukio lakini bado haja0ngea na vyombo vya habari.Mpaka sasa mlipuko huu chanzo chake hakijajulikana.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO