Thursday 16 May 2013

MAAJABU::WAOMBOLEZAJI WAKIMBIA JENEZA BAADA YA MAITI KUFUFUKA NCHINI ZIMBABWE

Waombolezaji katika msiba nchini Zimbabwe walipigwa na butwaa pale mtu aliyekufa alipoamka wakati wakipita kando ya jeneza lake kutoa heshima za mwisho, shirika la habari za nchi hiyo limeripoti jana.

Brighton Dama Zanthe, mwenye miaka 34, aliingizwa ndani ya jeneza Jumatatu iliyopita baada ya kuwa amefariki nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Familia iliyojawa na huzuni ya mfanyakazi huyo wa usafirishaji ilifunika mwili wake kwa mablanketi na kufanya mipango ya kumhamishia kwenye mochari ya mjini humo, kwa mujibu wa  ripoti iliyochapishwa katika gazeti la The Herald.

Lakini siku iliyofuata marafiki wa Zanthe na jamaa zake walisambaratika wakiwa hawaamini pale alipoanza kutembea wakati wakipita mbele ya jeneza kuaga mwili wa 'marehemu' huyo.
Bosi wa 'marehemu' huyo, Lot Gaka alieleza kuhusu mkasa huo alipobaini mfanyakazi wake alikuwa bado angali hai.

Alisema: "Kwanza niligundua miguu ya Zanthe ikisogea wakati nilipokuwa kwenye ya foleni kutazama mwili wake. Hili lilinishitua mno. Kwanza sikuweza kuamini macho yangu lakini baadaye nilibaini kwamba kulikuwa na kusogea kwa viungo kadhaa katika mwili wake huku waombolezaji wengine wakiwa hawaamini kinachoendelea."

Gaka, ambaye anaendesha kampuni ya mabasi katika mji wa Gweru, alisema Zanthe alikuwa hana afya njema kabla ya 'kifo' chake wiki iliyopita.
Alielezea minsi alivyotembelea nyumbani kwa familia hiyo kutoa msaada pale mke wa mfanyakazi wake alivyompigia simu kumweleza kwamba Zanthe alikuwa amefariki.
Alisema: "Zanthe alikuwa katika likizo ya ugonjwa kwa kipindi fulani na kila mmoja kazini alikuwa akifahamu kwamba hali yake ilikuwa mbaya.

"Tulimtembelea nyumbani kwake.
"Sikushangaa pale nilipopokea simu kutoka kwa mke wa Zanthe Jumatatu usiku wiki iliyopita akisema kwamba mume wake alikuwa amefariki."

Aliongeza: "Nilitembelea maduka mawili yanayouza majeneza mjini humo kwa ajili ya kuulizia gharama kabla ya kuelekea nyumbani kwa Zanthe hivyo kuweza kuchukua mwili wake na kuuhifadhi katika mochari.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO