Thursday 16 May 2013

UFAFANUZI WA ASKOFU MTEGA KUSTAAFU HUU HAPA

17.05.2013
Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo Katoliki la Songea Mhashamu NORBERT MTEGA amekutana na waandishi wa habari Mjini SONGEA Mkoani RUVUMA kwa lengo la kutoa ufafanuzi juu ya uamuzi wake wa kumuomba Baba Mtakatifu kustaafu na kusema amefanya hivyo kwa maslai ya jimbo kuu Katoliki la Songea baada ya kubaini kuwa afya yake haimwezeshi kumudu majukumu ya kiutawala ya jimbo hilo.



Aidha Askofu Mtega mwenye umri wa miaka 68 alisema licha ya kustaafu kwake ataendelea kufanya majukumu ya kitume kama kawaida na amechagua kuishi SONGEA baada ya kustaafu huku akitaka wakatoliki wa jimbo hilo wasiwe na wasiwasi na uamuzi wake



 Baada ya saa kadhaa za maombi ya wandishi wa habari waliokua na kiu ya kuzungumza na Askofu Mkuu Mstaafu NORBERT MTEGA juu ya uamuzi wake wa kuomba kustaafu na hatimaye kukubaliwa na Baba Mtakatifu PAPA FRANCIS, hatimaye wakakutana nae majira ya jioni, na kwanza ilikua ni kutaka ufafanuzi wa kwa nini amechukua hatua hiyo iliyoshitua watu wengi



Askofu akajibu kuwa yeye anajitambua kuwa hana afya nzuri itakyomwezesha kusimamia shughuli zote kwa ufanisi kwa kuwa kunahitaji kufikiri kwa hali ya juu.



 Pili, waandishi wa Habari wakata kujua kwa nini afanye hivyo wakati umri wake wa kustaafu kwa hiari ambao ni miaka 70 hajafikia, wala kustaafu kwa lazima ambao ni miaka 75 hajafikia



 Tatu, tukataka kujua Askofu Mtega angependa Askofu Ajae afanye nini kwa maslai ya jimbo kuu katoliki la Songea



Askofu Mtega akajibu kuwa askofu atakayefika aendeleze kuimarisha imani za waumini bila kusahau huduma za kijamii kama vile elimu na afya.



 Aidha Askofu MTEGA amesema hakuna lolote baya lilisababisha yeye astaafu kazi hii ya kuhudumia jimbo kuu katoliki la Songea ambalo kiutawala linasimamia majimbo nane a ya kusini mwa Tanzania



 Kabla ya kuagana na Askofu Mtega, ikawa ni swali la wapi ataishi wakati wa kustaafu



 Askofu Mstaafu Norbert Mtega atoa ufafanuzi kuwa anapenda kuendelea kuishi hapa Songea.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO