Thursday 16 May 2013

KIM AANIKA HADHARANI BUNDUKI 26 ZA TAIFA STARS KUWAKABILI MORROCO!!

   Mtibwa-Sugar

Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Wakata miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar chini ya kocha mkuu Merky Mexime wanatarajia kuwasili kesho jiji la Maji Chumvi, Dar es salaam tayari kwa kipute cha kufunga pazia la ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2012/2013  dhidi ya maafande waliohaha kiukweli kujinusuru na makasi wa kushuka daraja na hatimaye kufanikiwa, JKR Ruvu ya Mkaoni Pwani.

Meneja wa klabu hiyo, David Bugoya ameimbia FULLSHANGWE Kuwa wanawasili kesho mchana na jioni watapasha misuli kusubiri kipute cha kesho kutwa (Mei 18) mwaka huu katika uwanja wa Chamazi maeneo ya Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.

“Tumejiandaa kwa muda mrefu na hapo kesho tutafika na kumalizia mazoezi yetu Dar es salaam, kocha wetu amefanya marekebisho ya makosa yaliyokuwepo katika kikosi chetu hivyo tuna matumaini ya kufanya vizuri”. Alisema Bugoya.

Akizungumzia hali ya wanandinga wao, Bugoya alisema wachezaji wote wapo salama na hakuna majeruhi mpaka sasa, hivyo mwalimu anajua nini cha kufanya ili kupata kikosi cha kuwafunga JKT Ruvu wakiwa nyumbani kwao.

“Mchezaji wetu Hussein Javu sasa yuko fiti sana, mchezo uliopita alifunga mabao mawili, sasa yuko vizuri zaidi na tutamtumia ipasavyo katika mchezo wetu wa kesho kutwa uwanja wa Chamazi”. Alisema Bugoya.

Mtibwa Sugar  katika msimamo wa ligi kuu wapo nafasi ya 5 wakiwa na pointi 39 kibindoni, wakati wapinzani wao wa mwisho JKR Ruvu chini ya kocha mpya Keny Mwaisabula “Mzazi” wapo nafasi ya 10 na pointi 26.

Kwa upande wa kocha Keny Mwaisabula amesema kuwa kikosi kipo shwari na wamejiandaa vizuri kukabiliana na Mtibwa, lakini hesabu zake kubwa ni msimu ujao wa ligi ambapo ataiongoza timu hiyo kurithi mikoba ya kocha aliyejiuzulu kuifundisha klabu hiyo Charles Kilinda.

“Kikosi cha JKT Ruvu ni kizuri sana, kina wachezaji wanaojua soka, kinachokosekana ni kujiamini pamoja na kuwajenga kisaikolojia, kazi hii nitaifanya vizuri baada ya msimu huu kumalizika, ili kuhusu mchezo wa kesho kutwa tumejiandaa vizuri”. Alisema Mwaisabula.
Timu za Mgambo Shooting, Polisi Morogoro, Africa Lyon na Toto Africans zina hali ngumu sana na tunaweza kuzungumza mengine baada ya mei 18 mwaka huu kwa maana ya tatu kati ya hizo kushuka daraja na kutoa nafasi kwa Mbeya City, Rhino Rangers na Ashant United kucheza ligi hiyo baada ya kufanikiwa kupanda msimu huu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO