Saturday 4 May 2013

MANENO MENGINE YA JIDE

UCHOYO NI KITU KINGINE KIBAYA SANA

Naomba kuwashukuru wote mliochangia kuhusu ndoto kwa njia moja au nyingine.
Maoni yote yana umuhimu na kila moja lina faida yake
Ila kuna waliosema sio vizuri kusimulia ndoto.

Mimi kwa maoni yangu ni kuwa
Kuna watu wengi wana matatizo makubwa ambayo hawawezi kuyasema, Pengine katika kuchangia kwenu maoni wanapata nao mwanga kupitia yale ninayoyapitia mimi.

Sasa anapotokea mtu mmoja mwenye nguvu ya kuzungumza anakuwa kawasaidia na wengine wenye kutaka kufahamu lakini hawajui wamuelezee nani?
Sidhani kama kuna ubaya niki share jambo na watu.

Uchoyo ni jambo baya sana, sasa uchoyo mpaka wa story tu jamani??
Kuna vitu vingi sana nimegundua naweza kujifunza kupitia maoni, Kuliko kukaa na vitu moyoni mwisho umauti.

Nitaendelea ku share chochote ninachohisi kinanisumbua ili nipate ufumbuzi, Hakuna ubaya unaoshinda nguvu ya MUNGU.

Hata bila kusimulia au kabla sijaanza kusimulia ndoto mbona bado kuna ubaya  ulikuwa unaendelea tu.

Sidhani nitamzuia mbaya, kunifanyia ubaya kwa kukaa kimya
Ubaya umefanywa miaka nenda rudi kabla sijasimulia lolote.
Na bado unaendelea kufanywa kwa vificho na hadharani.

Ni MUNGU tu amesimamia kati kati pale.

Nina story nyingine ya kutisha nitakuja kuwasimulia hamtaamini ila ndio dunia. Kwa wengine wenye makubwa kuliko hivi viji story vyangu, Pls stay strong. Na msisite ku share ili wanaosoma wapate kujifunza kuwa unaweza kukutana na magumu na bado ukapumua.

Kuna muda wa ushindi unakuja.
Hakuna mateso yasio na mwisho,
Hata kama mwisho ukiwa ni kifo.

Kwa leo niishie hapa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO