Wednesday 8 May 2013

SIMBA YAIFUMUA MGAMBO JKT BAO 1-0

Timu ya SIMBA imeendelea kufanya kweli katika ligi baada  ya Haruna Chanongo kufunga Bao katika Dakika ya 8 na kuipa ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na Mgambo JKT kwenye Mechi ya VPL, Ligi Kuu Vodacom, iliyochezwa  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
 
Simba wakiwa wamebakisha Mechi moja, ile Dabi ya Kariakoo, na Mahasimu wao Mabingwa Yanga hapo Mei 18, wapo nafasi ya 3 Pointi 3 nyuma ya Timu ya Pili Azam FC ambao wana Mechi mbili zilizobaki.
Tayari Yanga wameshatwaa Ubingwa na Msimu ujao watacheza CAF CHAMPIONZ LIGI na Mshindi wa Pili, Azam FC au Simba, watacheza CAF Kombe la Shirikisho.

Wakati Simba wamebakisha Mechi 1 tu ya kucheza na Yanga Siku ya mwisho Mei 18, Azam FC, Jumamosi Mei 11, watakuwa kwao Azam Complex, Chamazi kwenye Viunga vya Dar es Salaam, kucheza na Mgambo JKT na Mei 18 kumaliza ugenini na JKT Oljoro huko Arusha.  

VIKOSI:
SIMBA: Juma Kaseja, Nassor Masoud ‘Chollo’, Haruna Shamte, Miraj Adam, Hassan Khatib, Jonas Mkude, Edward Christopher, William Lucianl, Amri Kiemba, Ramadhani Singano, Haruna Chanongo.
JKT MGAMBO: Godson Mmasa, Salum Mlima, Ramadhani Kambwili, Bashiru Chanacha, Bakari Mtama, Salum Kipanga, Chande Magoja, Peter Mwalyanzi, Issa Kandulu, Fully Maganga, Nassor Gumbo.
 
RATIBA:

Jumamosi Mei 11
Azam FC Vs Mgambo JKT
Kagera Sugar Vs Ruvu Shooting
Jumamosi Mei 18
Toto Africans Vs Ruvu Shooting
Mgambo JKT Vs African Lyon
JKT Ruvu Vs Mtibwa Sugar
TZ Prisons Vs Kagera Sugar
Simba SC Vs Yanga SC
JKT Oljoro Vs Azam FC
Polisi Moro Vs Coastal Union
MSIMAMO:
YANGA BINGWA
NA TIMU P W D L GF GA GD PTS
1 YANGA 25 17 6 2 45 14 31 57
2 AZAM FC 24 14 6 4 42 20 22 48
3 SIMBA SC 25 12 9 4 38 23 15 45
4 KAGERA SUGAR 24 11 7 6 25 18 7 40
5 MTIBWA SUGAR 25 10 9 6 29 24 5 39
6 COASTAL UNION 25 8 11 6 25 23 2 35
7 RUVU SHOOTING 24 8 7 9 21 23 -2 31
8 JKT OLJORO 25 7 8 10 21 26 -5 29
9 TANZANIA PRISONS 25 7 8 10 16 22 -6 29
10 JKT RUVU 25 7 5 13 21 38 -17 26
11 MGAMBO SHOOTING 24 7 4 13 16 24 -8 25
12 POLISI MOROGORO 25 4 10 11 13 23 -10 22
13 TOTO AFRICAN 25 4 10 11 21 33 -12 22
14 AFRICAN LYON 25 5 4 16 16 38 -22 19
AFRICAN LYON IMESHUKA DARAJA

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO