Saturday 4 May 2013

MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATANGAZA KUFUNGUA MGODI WA MAKAA YA MAWE ULIOFUNGWA SIKU CHACHE ZILIZOPITA

                                                                    picha siyo ya tukio

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma atangaza kufungua mgodi wa makaa ya mawe alioufunga siku chache zilizopita huku akitoa siku 45 kwa kampuni ya TANCOAL kulipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa fidia zao na katoa siku 14 kuhakikisha vyanzo vya maji vyoe vilivyokuwa vinachafuliwa na shughuli za uchimbaji zinakuwa salama.

Mgodi wa makaa ya mawe upo katika kijiji cha Mtunduwalo katika wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma ambao muda si mrefu unatarajia kuanza kuzalisha umeme utakaounganishwa kwenye gridi ya Taifa na wakazi wa mkoa wa Ruvuma hawatapata tabu ya umeme tena.


No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO