Friday 31 May 2013

Mrehemu Ernest Zulu azikwa Maposeni Songea


Na Nathan Mtega,Songea


MWILI wa marehemu aliyekuwa mwandishi wa vikao vya Bunge la Tanzania Ernest Zulu umezikwa katika makaburi ya kichifu yaliyopo Maposeni Peramiho wilayani Songea mkoani Ruvuma huku mazishi hayo yakifanyika bila kuhudhuriwa na familia yake jambo ambalo liliwashangaza baadhi ya watu waliohudhuria mazishi hayo.

  Wakiongea kwa sauti za chini kwenye mazishi hayo baadhi ya wakazi wa Peramiho walisema kuwa wameshangazwa kuona wasifu wa marehemu ukisomwa na kuonyesha kuwa marehemu amewaacha watoto wanne na mke mmoja lakini cha ajabu hawaonekani kwenye msiba huo.

      Kwa upande wake kaka wa marehemu  chifu Emmanuel Zulu akiwashukuru mamia ya watu walioshiriki kwenye mazishi hayo akiwemo akiwemo  Mbunge aliyetumwa na bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuja kuwakilisha mazishi hayo Abdukalim Shaha wa jimbo la Mafia Zanzibar alisema kuwa yeye hana  cha zaidi ya kumshukuru Mungu aliyetenda mambo hayo.

      Aidha kwa upande wake Mbunge Abdukalim Shaha akitoa salaamu za bunge amewataka viongozi wa dini zote kuendelea kujenga mshikamano wa kuliombea taifa lisiingie kwenye machafuko maana amani ikitoweka hakuna atakayekuwa huru kwa kufanya kazi zake.

        Alisema kuwa marehemu Ernest Zulu alitokea katika familia ya kichifu lakini kafanya mambo mazuri mengi katika taifa kwa sababu wazazi wake walikuwa wakihimiza amani na utulivu vidumu siku zote na siyo vinginevyo hivyo jamii inapaswa kuiga na kuendeleza moyo huo wa uzalendo.

        Alisema kuwa hali ya sasa  inayojitokeza katika vikao vya bunge kwa baadhi ya viongozi kutaka kushikana mwilini hivyo ni vyema jamiin kwa ujumla ikasaidiana kumuomba Mungu aweze kuepusha balaa hasa kwa kuwakemea vijana waachane na ushabiki usiyokuwa wa msingi.

      Hata hivyo aliipongeza ofisi ya mkuu wa wilaya ya Songea kwa kazi nzuri ya kufanikisha maandalizi ya mazishi hayo kwa kuwapokea wageni na kufanikisha kuwapa huduma na kuwa hiyo wanaenda kuiweka kwenye rekodi ya ofisi ya Mbunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    Lakini pamoja na wakazi hao kuhudhuria kwenye mazishi hayo wakiwemo viongozi wa safari ya mwisho ya Ernest Zulu lakini wananchi hao walionyeshwa kutoridhika kwa kutokuwepo Mbunge hata mmoja wa mkoani hapo zaidi ya wawakilishi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAONI YAKO